Kocha wa kikosi cha Mamelodi Sundowns Rulani Mokwena ameweka wazi kuwa wana kawaida ya kukagua uwanja kabla ya mechi bila viatu na sio imani za kishirikina.
"Huwa binafsi mimi na wachezaji wangu tunatembea bila viatu wakati tunapoukagua uwanja wa wapinzani wetu."
"Wasiotufahamu haswa katika michezo ya kimataifa wanahisi ni uchawi wetu ila ukweli ni kwamba huwa tunafanya hivyo kwa faida za kisayansi na sio uchawi."
"Kisayansi, inaelezwa kwamba faida mojawapo ya kutembea Peku ama bila viatu huruhusu mwili kuchukua elektroni za bure kutoka kwa ardhi kupitia nyayo za miguu."
"Hii husaidia kupunguza kuvimba na kuondoa ama kupunguza hisia za uwoga kwa mtu mgeni."
Mamelodi Sundowns itakipiga na Yanga Jumamosi hii katika dimba la Benjamin Mkapa, kwahiyo msishangae kuwaona wakitembea peku wakati wa ukaguzi wa uwanja.