Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mamelodi vs Wydad hapatoshi Fainali AFL leo

Mamelodi Vs Wydad First Leg Mamelodi vs Wydad hapatoshi Fainali AFL leo

Sun, 12 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mashabiki wa soka barani Afrika kuanzia saa 10:00 jioni watakuwa bize kufuatilia pambano la pili la fainali ya African Football League wakati Mamelodi Sundowns itakapokuwa nyumbani kurekebisha makosa ya mechi ya mkondo wa kwanza mbele ya Wydad Casablanca

Katika mechi ya kwanza wikiendi iliyopita, Wydad ikiwa nyumbani, ilishinda 2-1 na kujiweka nafasi nzuri ya kuandika historia ya kuwa bingwa wa kwanza wa michuano hiyo, iwapo itashikilia bomba kwenye Uwanja wa Loftus Verfeld, mjini Pretoria.

Ushindi hata wa bao 1-0 unaweza kuwabeba wenyeji, lakini kwa jinsi Wydad ilivyoupiga mwingi kwenye michuano hiyo hadi sasa ni wazi, Mamelodi wana kazi ya ziada kama inataka kulibeba taji hilo ambalo Wekundu wa Msimbazi, Simba walishiriki na kung’olewa na Al Ahly.Huo ni mchezo wa 14 kwa timu hizo kukutana kwenye michuano ya CAF, huku Wydad ikiwa na rekodi nzuri.

Nani atabeba ndoo ya AFL leo

Chanzo: www.tanzaniaweb.live