Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mamelodi kutua na Mashabiki 400, kuja na Ulinzi maalum

Mashabiki Wa Mamelodi Fans Mashabiki wa Mamelodi Sundowns

Mon, 25 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kitendo cha Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuandika barua kwenda kwa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuijulisha, mechi hiyo itachezwa kwa kufuata kanuni na taratibu za soka zilizowekwa, kimeonekana kuwapa mzuka mashabiki wa Mamelodi wanaotarajia kusafirisha idadi kubwa ya mashabiki wao kuja nchini kuwaunga mkono katika mechi hiyo.

Timu hiyo inaripotiwa kuomba nafasi ya mashabiki wapatao 400 kwa ajili ya kuingia katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, kuishangilia. Inadaiwa, Mamelodi ilionyesha wasiwasi wa kusafirisha mashabiki wake kuja nchini kushuhudia mechi hiyo, baada ya kauli iliyotolewa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Damas Ndumbaro, ili shabiki wa timu pinzani ya Simba au Yanga aruhusiwe kuingia uwanjani katika mechi hizo za mwishoni mwa wiki ijayo, anapaswa kuonyesha hati yake ya kusafiria ya nchi inazotoka timu hizo.

Taarifa pia zinasema Mamelodi imeamua kuja na walinzi maalumu ambao jukumu lao ni kuhakikisha hakuna mwingiliano wowote kati yao na wachezaji wa timu hiyo pindi watakapokuwa hoteli au uwanjani wakati wa mechi na mazoezi.

Timu hiyo pia imepanga kutotumia usafiri wa basi ambao Yanga imeuandaa kwa ajili yao katika kipindi chote itakachokuwepo hapa nchini na itajigharimia na kuandaa usafiri wake na tayari imeshatanguliza maofisa wa awali hapa nchini kwa ajili ya kuweka mambo sawa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live