Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mamelodi hawauzi silaha kwa adui kizembe

Mokoena South Africa Mamelodi hawauzi silaha kwa adui kizembe

Wed, 15 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hakuna mazungumzo yoyote ya kumsaini kiungo wa Mamelodi Sundowns, Teboho Mokoena kwenda Al Ahly lakini kukitokea nafasi ya kufanya hivyo basi Al Ahly hawataipoteza.

Mamelodi ni moja ya vilabu vinavyopigania makombe Afrika hivyo haiwezekani wao kukubali kuwauzia Ahly mchezaji mzuri kama Mokoena.

Teboho Mokoena ambaye ni kapteni msaidizi wa Mamelodi tayari ameongeza mkataba mpya wa kuendelea kuwatumikia Mamelodi Sundowns kwa miaka miwili hadi mwaka 2026.

Mbali na mkataba huo Al Ahly SC wamesema watauvunja mkataba huo kwa gharama yeyote ile.

Kipindi Kocha Pitso yuko Misri na Al Ahly, waliwahi kujaribu kumsaini Sirino kutoka Mamelodi Sundowns lakini walijataa katukatu kwa sababu hawataki kumuuza mchezaji zaidi ndani ya Afrika hasahasa kwa wapinzani wao wakubwa Al Ahly ambao wanapambana nao.

Hadi Sasa Al Ahly hawajaamua kuhusu wachezaji wapya lakini kuna pendekezo la Marcel Koller (Kocha wa Ahly) kusajili wachezaji wawili nje ya Egypt.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live