Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mamelodi Sundowns yatema wanne

Mamelodi 3wK.jpeg Mamelodi Sundowns yatema wanne

Mon, 1 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Mamelodi Sundowns imeachana rasmi na wachezaji wao wanne kwenye kikosi hicho.

Wachezaji hao ni;

1. Leonardo Gaston Sirino Rodriguez (33), kiungo mshambuliaji raia wa Uruguay ambaye alijiunga na Mamelodi mwaka 2018 akitokea Bolivar. Kiungo huyo pia anahusishwa kujiunga na klabu ya Wydad Casablanca ya nchini Morocco.

2. Brian Mandela Onyango (29), mlinzi wa kati raia wa Kenya ambaye ni mchezaji huru kwa sasa

3. Thabiso Kutumela (30), mshambuliaji ambaye alipelekwa kwa mkopo klabu ya Capetown City. Thabiso alijiunga na Mamelodi mwaka 2021akitokea Maritzburg United na Sasa ni mchezaji huru.

4. Bongani Zungu (31), kiungo wa ulinzi ambaye alijiunga na Mamelodi mwaka 2022.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live