Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mamelodi Sundowns waichapa Cotton Sports ugenini

Cotton Sports Vs Mamelodi Mamelodi Sundowns waichapa Cotton Sports ugenini

Sat, 18 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Miamba ya Soka kutoka Afrika Kusini, Mamelodi Sundowns wameibuka na ushindi wa mabao 3-1 ugenini dhidi ya Cotton Sports katika dimba la Roumde Adja, Garoua, Cameroon.

Mchezo huo wa kundi B, uliwashuhudia wageni wakipata mabao matatu ndani ya dakika 45 za kipindi cha kwanza yakifungwa na C. Mailula aliefunga mabao mawili dakika za 10 na 43 huku T. Morena akifunga bao moja dakika ya 11.

Bao pekee la Cotton Sports limefungwa na P. Wassou dakika ya 32.

Kwa ushindi huo Mamelodi wanafikisha alama 6 baada ya michezo miwili wakiongoza kundi B.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live