Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mamelodi; Sauti ya Mama wa Afrika na Ufalme wake wa soka la kibabe

Mamelodi Sundown 68.heic Mamelodi Sundown.

Thu, 14 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kabla ya ujio wa midundo ya Amapiano, Wasouth Afrika walifurahishwa zaidi na

Orlande Pirates na Kaizer Chiefs.

Wakati mboni zetu zikiwa zinashuhudia anguko la Orlando Pirate na Kaizer Chiefs miaka ya 2000. Mamelodi Sundown walikuwa "busy" kusuka mipango ya kijasusi ya kuliteka bara la Afrika Kisoka.

Wakati huu mamelodi wakiwa kileleni mwa Ligi Kuu ya Dstv kwa tofauti ya point 12 huku wakiwa na michezo miwili mkononi.

Hawajafungwa kwenye ligi yao kwenye michezo 41, Ni muendelezo wa mipango ya kijasusi ya kuliteka soka la Afrika ulioanzishwa mwaka 2004 baada ya timu hiyo kuangukia kwenye mikono ya tajiri Dr Patrice Motsepe.

Kama ilivyo kwa GSM na Mo Dewji, hivyo hivyo kwa Patrice Motsepe hajawahi kuchoka kuvujisha mfuko wake kwenye usajili na kuleta wachezaji au kocha bora.

Licha ya matumizi makubwa ya fedha lakini mamelody Sundown safari yake ya mafanikio haikuwa rahisi, upo mwaka Dr Patrice Motsepe alijaribu kuchukua makocha kutoka Barcelona, Hristo Stoickhov pamoja Johan Neeknes na haikulipa.

Yupo kocha wa kifaransa aliyeishia kuondolewa kwa kusindikizwa na polisi baada ya vurugu za mashabiki kwa sababu ya matokeo mabovu, Henry Michel. Mambo hayakuwa kama alivyotaka Dr Pateice Motsepe hadi alipofika Pitso Mosimane mwaka 2012.

Ni ubongo wa Pitso Mosimane ndio ulianza kuwatia jeuri mashabiki wa Mamelody Sundown. Mwaka 2016 aliiwezesha Mamelody Sundown kubeba Caf Champion league kwa kuichapa Zamalek na kuifanya Mamelody Sundown kuwa timu ya pili kutoka south Afrika kuchukua kombe hilo tangu mwaka 1995, Orlande Pirates walipofanya hivyo.

Miaka 6 ya Pitso Mosimane, ilitosha kuvunja utawala wa timu nyingi babe Afrika. 'Ma' kwa lugha ya sepedo inamaana ni 'Mama'. Na melodi ni sauti. Hivyo Mamelodi ni Mama wa Sauti.

Wakati huu tukiwa na shauku ya kuiona Mamelody sundown Benjamini mkapa stadium unadhani ni timu ipi ya kariakoo itaweza kuisimamisha mamelody Sundown ''Masandawana"?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: