Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mamelodi, Al Ahly zinafungika kazeni watani

Simba Yanga WA0007 Mamelodi, Al Ahly zinafungika kazeni watani

Fri, 15 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Jumanne iliyopita, droo ya hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu ilipangwa kibabe sana pale Cairo, Misri.

Yanga ilijikuta ikipangwa kukutana na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini wakati Simba yenyewe iliangukia mikononi mwa Al Ahly ya Misri huku timu zote hizo za Tanzania zikipangwa kuanzia nyumbani.

Ni timu dume kweli ambazo zimepangwa na wawakilishi wetu kutokana na historia zilizonazo kwenye soka la Afrika na uwekezaji ambao zimefanya kwa muda mrefu.

Al Ahly ndio klabu iliyofanikiwa zaidi barani Afrika kulinganisha na nyingine kutokana na idadi kubwa ya mataji ambayo imechukua na mfano ni la mabingwa Afrika ambalo imelitwaa mara 11 ambazo ni nyingi zaidi kuliko klabu nyingine.

Ukiizungumzia Mamelodi Sundowns, unaigusa timu ambayo hivi karibuni imetwaa ubingwa wa mashindano mapya ya African Football League (AFL) huku ikionyesha soka safi na la kuvutia pengine kuliko timu nyingine yoyote kwa sasa.

Homa ya mechi za hatua ya robo fainali ni kama imeshaanza kupanda kwa timu zetu na wengi wamekuwa katika hofu kwamba hatua hiyo inaweza kuwa mwisho wa ushiriki wa timu za Tanzania.

Hata hivyo, mimi sioni haja ya timu zetu kuogopa kukutana na Mamelodi Sundowns na Al Ahly kwani ni timu ambazo zinaweza kufungika ikiwa klabu zetu zitajipanga vizuri kabla ya kukabiliana nazo.

Eneo ambalo timu zetu zinapaswa kulifanyia kazi kikamilifu ni la mbinu ambapo zinapaswa kujiimarisha vilivyo ili zipate mpango bora wa kuzikabili timu hizo mbili kubwa barani Afrika.

Zipo mechi ambazo tumeshuhudia Mamelodi Sundowns na Al Ahly zimefungika na hilo lilitokana na maandalizi mazuri ya hizo timu ambazo zilicheza nazo hivyo Simba na Yanga zinaweza kama zikijipanga vilivyo.

Chanzo: Mwanaspoti