Coton Sport ndio vibonde kwenye Kundi B, imepoteza michezo yote mitatu (3) iliyopita, leo inakutana na Al Hilal ambayo tayari imeshashinda mechi zake mbili, endapo Al Hilal itashinda leo itafikisha alama tisa (9) na kuendelea kuikimbia Al Ahly ambayo ina alama nne (4).
Hili ni miongoni mwa makundi magumu kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, vigogo watatu [Mamelodi Sundowns, Al Hilal na Al Ahly] wanapambana kuitafuta Robo Fainali.
MSIMAMO KUNDI B
Mamelodi——[7] pts
Al Hilal———[6] pts
Al Ahly———[4] pts
Coton Sport—[0] pts
Wakati Al Hilal wakiwa nyumbani kucheza na Coton Sport, wanajua mechi zao dhidi ya Mamelodi na Al Ahly zitakuwa ngumu sana kwa vyovyote vile leo watakomaa ili wapate alama tatu (3) ili wafikishe alama tisa (9).
Mamelodi pia watakuwa nyumbani kuwakabili Al Ahly, kwa namna yoyote hawa watapunguzana, timu moja inaweza kuchukua alama zote tatu (3) au kugawana alama moja moja.
Ikitokea Al Hilal ikashinda, halafu Al Ahly ikaifunga Mamelodi maana yake Al Hilal itaongoza Kundi kwa kufikisha alama tisa (9) halafu Mamelodi na Al Ahly kila timu itakuwa na alama saba (7). Mamelodi na Al Ahly zikitoka sare Mamelodi itafikisha alama nane (8) na Ahly alama tano (5). Kundi litakuwa gumu sana!!
Mamelodi wakiifunga Al Ahly watafikisha alama 10, Al Ahly itaendelea kubaki na alama nne (4) na mambo yatazidi kuwa magumu kwao.