Huu ni Msimu 2023-24 unaonekana kuwa msimu mchungu Kwa Manchester United ikiwa chini ya Kocha mkuu Erik Ten Hag.
Yale matumaini ya mashabiki wa United waliyoyapata msimu uliopita baada ya kumaliza nafasi ya tatu katika msimamo wa Premier kwa sasa mambo yamekuwa ni tofauti na wengi walivyokuwa wakitarajia
Miongoni mwa mechi saba ambazo wamecheza mpaka sasa katika michuano yote, wameshinda mechi tatu tu na kupoteza mechi nne.
Mpaka Sasa United imefanikiwa kufunga mabao 10, wakiruhusu mabao 14, ikiwa bado wapo katika rekodi mbovu.
Kwa sasa inasemekana kama matokeo yataendelea kuwa mabaya zaidi ndani ya United, inawezekana Ten Hag akapewa mkono wa kwaheri ndani ya klabu hiyo huku akitafutiwa atakayekuwa mrithi wa mikoba yake.