Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mambo yakuangalia Ligi Ikirejea leo

Geita Gold Vs Tbatora.jpeg Mambo yakuangalia Ligi Ikirejea leo

Wed, 22 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya kupisha michezo ya kimataifa, hatimaye Ligi Kuu Bara inarejea tena leo Jumatano kwa michezo miwili kupigwa ambapo Geita Gold itakuwa Uwanja wa Nyankumbu kucheza na JKT Tanzania huku Kagera Sugar ikiikaribisha KMC Uwanja wa Kaitaba.

Wakati ligi hiyo inarejea yapo mambo ya kuangalia kwa timu zinazocheza hasa baada ya miamba ya soka nchini Yanga ambayo iko kileleni mwa msimamo na Simba ambazo zote zinashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika hazitokuwa na mchezo hadi Desemba.

Jambo la kwanza linaloweza kutokea ni kwa Azam yenye pointi 19 ina uwezekano mkubwa ikafikia pointi 24 za Yanga ikiwa itashinda michezo yake miwili tu sawa na Dodoma Jiji na KMC ambazo nazo pia zimejikusanyia pointi 15 kila mmoja wao.

Mtibwa Sugar inayoburuza mkia na pointi tano itakuwa na kazi ya kujinasua nafasi hiyo sambamba na Geita Gold na Tanzania Prisons ambazo kila mmoja imekusanya pointi saba katika michezo tisa iliyocheza hadi sasa.

Kwenye ufungaji nako kutakuwa na kazi ya ziada ambapo washambuliaji watakuwa na kibarua cha kuwafikia Stephane Aziz Ki na Maxi Mpia Nzengeli wa Yanga na Jean Baleke wa Simba ambao nyota hao kila mmoja wao amefunga mabao saba hadi sasa. Nyota wanaoweza kufikia mabao saba ni Fei Toto wa Azam aliyefunga matano, Marouf Tchakei wa Singida Big Stars mwenye manne na Matheo Anthony (Mtibwa Sugar), Prince Dube (Azam) na Waziri Junior wa KMC wenye matatu kila mmoja.

Kocha wa Kagera Sugar, Mecky Maxime alisema; “Mwanzoni unapokuwa unacheza nyumbani inakuwa ni faida kwako kujihakikishia kubaki na pointi tatu lakini kwa msimu huu bila ya maandalizi unafungwa popote,” alisema.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: