Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mambo yaanza kuwa magumu kwa Nabi, Morocco

Nabi Tres Mambo yaanza kuwa magumu kwa Nabi, Morocco

Tue, 5 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mambo yameanza kuwa magumu kwa aliyekuwa Kocha wa yanga SC, Nasreddine Nabi baada ya kupata sare ya kwanza katika mchezo wa pili tu wa Ligi Kuu ya Morocco 'Botola Pro League'.

Nabi amejiunga na FAR Rabat msimu huu akitokea Yanga baada ya kupata mafanikio makubwa nchini Tanzania alipoitumikia Klabu hiyo kwa miaka miwili.

Mchezo wa kwanza wa Ligi ya Morocco, Far Rabat ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi hiyo walishinda bao 2-0 dhidi ya Chabab Mohammedia wakati mchezo wa pili dhidi ya Raja Club Athletic ametoa sare hiyo ya bao 2-2.

FAR Rabat wameanza Ligi namna hii;

◉ Far Rabat 2 - 0 Chabab

◉ Raja Club Athletic 2 - 2 Far Rabat

Raja wameanza ligi namna hii;

◉ Youssofia 1 - 3 Raja Athletic

◉ Raja Club Athletic 2 - 2 Far Rabat

Timu zote zimecheza mechi mbili.

1. Pts 6 — UTS

2. Pts 6 — RS Berkane

3. Pts 6 — JS soualem

4. Pts 4 — Raja Club Athletic

5. Pts 4 — FAR Rabat

9. Pts 3 — Wydad Casablanca

Nabi ana jukumu la kutetea Ubingwa wa ligi kuu ya Morocco na kuwavusha FAR Rabat hadi fainali CAF Champions League.

Raja Casablanca msimu uliopita walimaliza patupu, nje ya top four na hata kwenye fainali ya (FA) dhidi ya RS Berkane ambao nao walimaliza nje ya top four walipoteza.

Raja msimu huu hatashiriki michuano ya (CAF), anakomaa na ligi kuu, Berkane yeye alipenya (CAF) kupitia (FA).

Ikumbukwe kuwa, Nabi akiwa Yanga amewahi kuweka rekodi ya kumaliza Ligi bila kufungwa huku pia akiweka rekodi ya kutofungwa mechi 49 za Ligi mfululizo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live