Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mambo sita niliyoyaona Taifa Stars vs Ethiopia

Taifa Stars AAATSDG.jpeg Mambo sita niliyoyaona Taifa Stars vs Ethiopia

Thu, 5 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imepata alama moja baada ya kutoka suluhu ya bila kufungana dhidi ya Ethiopia kwenye machezo wa kuwania kufuzu michuano ya AFCON 2025.

Taifa stars ikiwa nyumbani kwenye dimba la Benjamin Mkapa, imeshindwa kufurukuta na wakiambulia alama moja pekee.

Stars imepangwa Kundi H pamoja na mataifa ya DR Congo, Guinea Tanzania na Ethiopia. Mchezo unaofuata kwa Stars watacheza ugenini dhidi ya Guinea.

1. Matokeo hayajawa ya kushangaza, Perfomance ya Ethiopia mbele ya Stars wala sio story. Stori inaweza kuwa How Moroco aliamua kuanza na player wengi wenye mentallity ya kuzuia (Zimbwe, Job, Bacca, Mao, Nova, Kibabage na Lusajo).

2. Bravo Ethiopia Benjamini Mkapa walikuwa wanatamba kama vile wapo Adis Ababa, Walikuwa na mechi bora katika nyakati zote mbili (Bila mpira pamoja na wakiwa na mpira) Good transition, confidency, exposure, Injurance na ftiness ya hali ya juu sana.

3. Hemed Moroco ni uoga wake tu, Lakini timu ya kushindana na Ethiopia alikuwa nayo. Tazama baada ya mabadiliko ya Mudathir Yahya, Pascal Msindo na Waziri Junior namna yalivoenda kuipa uhai Stars katika ile robo tatu ya mwisho kuelekea kwa wapinzani wao.

4. Ule muhimili wa Stars una ukomavu wa hali ya juu sana, Unavumilivu mno, Mstari wa safu ya ulinzi na kiungo wanacheza wakiwa karibu karibu sana pamoja na kusawazishiana makosa, Shida kubwa ni katika robo tatu ya mwisho haswa first half Fei, Balua na Kibabage walishindwa kabisa kutengeneza nafasi kwa Clement Mzize.

5. Mudathir Yahya Abas kiungo kisheti wa boli, Anakupa faida timu ikiwa na mpira anakuwa namba kumi wapili, Timu bila mpira anakuwa namba sita wa pili. Baada ya kuingia alibadili taswira ya mchezo kwa kiasi kikubwa sana haswa kutokana na utulivu wake katika dimba la kati ni presser mzuri pamoja na passer mzuri sana, Good game kutoka kwake.

6. Halafu pale dimba la kati Waethiopia walikuwa na mtu wakuitwa Gatuoch Panom Yiech. mmmh alikuwa mwalimu haswa akiwafunza vijana kazi za kiume. Kakichafua sana, kavuja sana jasho. Alikuwa na good perfomance hakika kitamba cha kuwa kiongozi anastahili kwakuwa alikuwa mfano mzuri kwa wenzake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live