Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mambo saba Ligi Kuu Bara

Yanga Azam F Mambo saba Ligi Kuu Bara

Fri, 27 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ligi Kuu Bara msimu huu imeanza na utofauti wake lakini kubwa zaidi ni namna ushindani ulivyokuwa mkali kwa timu ngeni ambazo ndio zimepanda kucheza ligi hiyo msimu huu tofauti na misimu mingine.

Baadhi ya timu kama KMC, Mtibwa Sugar na Tabora United zilianza kwa kupokea vichapo huku Ihefu ikiendeleza alipoishia msimu uliopita kwa kuifunga Yanga mabao 2-1, ikiwa ni kati ya matokeo ya kushangaza msimu huu.

Mwanaspoti kupitia makala haya linakuletea mambo saba yaliyotokea kwenye ligi hiyo inayoshika nafasi ya tano Afrika hadi sasa.

MASHUJAA YARUHUSU MABAO TATU

Mashujaa ni miongoni mwa timu zilizopanda daraja Ligi Kuu msimu huu lakini imeanza kuonyesha ushindani mkali, mpaka juzi ilipokuwa inacheza na Coastal Union ilikuwa imeruhusu bao moja.

Timu hiyo imecheza mechi sita, tatu nyumbani, tatu ugenini imepoteza mbili na kutoka suluhu moja, lakini jambo la ajabu ni kwamba pamoja na kwamba ni timu ngeni kwenye ligi hadi sasa imeruhusu kufungwa mabao matatu tu.

Mashujaa mpaka sasa ndio timu iliyoruhusu mabao machache iliporuhusu nyavu za kutikiswa na JKT Tanzania ugenini na Coastal Union kwa mabao 2-0. Ikifuatiwa na vigogo Simba na Yanga ambao wote wameruhusu mabao manne.

Kwenye mechi hizo, Mashujaa imefunga mabao manne pekee wastani wa chini ya goli moja kwa kila mechi.

MTIBWA HALI TETE

Mtibwa Sugar ina hali tete mpaka sasa kwani kwenye mechi sita za ligi haijaonja ushindi wa aina yoyote hadi kufikia kuachana na kocha wake.

Safu ya ushambuliaji ya timu hiyo siyo mbaya sana kwani kwenye michezo hiyo sita imefunga mabao sita na kuwa na wastani wa kufunga angalau bao moja kwa kila mechi.

Mabao sita iliyofunga, matatu yamefungwa na straika mmoja, Matteo Anthony huku matatu yakifungwa na viungo.

Hata hivyo, msimu huu Mtibwa imepandisha wachezaji wengi waliofanya vizuri kwenye timu ya vijana U-20 lakini wameonekana kutokuwa na uwezo wa kuisaidia timu hiyo kwenye ligi.

Huenda tatizo la mabeki likawa sababu ya wachezaji kuruhusu mabao mengi kwa kukosa uzoefu kwenye kikosi cha wakubwa.

Mabeki wa timu hiyo wameruhusu mabao 12 sawa na Tanzania Prisons ikiwa ni uwiano wa kuruhusu mabao mawili kwa kila mechi.

Ilianza kwa kufungwa mabao 4-2 na Simba nyumbani, 1-1 na Coastal Union, 1-1 na Dodoma Jiji ugenini, ikafungwa bao 1-0 na Singida BS nyumbani, Tanzania Prisons 3-2 ugenini na kumaliza na Kagera Sugar kwa mabao 2-0.

Prisons nayo imeruhusu mabao 12 lakini angalau ina wastani mzuri wa kufunga bao moja kwa kila mechi licha ya kufungwa mabao mengi lakini imefunga saba.

NNE ZAONGOZA KWA SARE

Timu nne zinaongoza kwa kupata sare zaidi ya mara moja huku Simba na Yanga zikiukimbia mtego huo.

Timu zilizopata sare nyingi ni Coastal Union, Namungo, Dodoma Jiji, na Tabora United ambazo zote zimepata sare tatu, huku KMC, Singida BS, Mashujaa, Kagera Sugar, JKT Tanzania, Tanzania Prisons na Mtibwa zikiambulia mbili.

SIMBA FRESHI

Achana na matokeo ya kimataifa ambayo Simba imekuwa ikiyapata kwa siku za hivi karibuni hata kwenye ligi imeendelea pale ilipoishia msimu uliopita na mpaka sasa ipo freshi.

Simba ndio timu iliyoshinda michezo yake yote mitano kwenye timu 16 za Ligi Kuu huku mtani wake Yanga akipoteza mmoja dhidi ya Ihefu kwa mabao 2-1 ugenini.

Vigogo watatu kwenye msimamo wa ligi ndio wanaongoza kwa kushinda mechi nyingi, Yanga na Azam FC zikipoteza mchezo mmoja kila mmoja huku Singida ikipoteza miwili.

RATIBA YAIBANA SIMBA, JKT

Mpaka mzunguko wa sita ni Simba na JKT pekee ndizo zilizocheza mechi mbili za nyumbani huku timu 14 zikiwa zimecheza mchanganyiko wa nyumbani na ugenini.

Baadhi ya timu kama Yanga, Ihefu, Namungo na nyingine zimeshacheza mechi nne nyumbani na mbili ugenini na wengine tatu nyumbani na tatu ugenini.

MSIMAMO ULIVYO

Kutokana na msimamo ulivyo sasa kwenye mechi sita ni Mtibwa Sugar na Coastal Union ambazo zinashuka daraja huku Namungo na Tanzania Prisons zikicheza playoff ili moja ishuke na mmoja iendelee.

Yanga inaongoza msimamo wa ligi kwa kucheza mechi sita na point 15 sawa na Simba ambayo ina mchezo mmoja mkononi huku Azam FC ikiwa nafasi ya tatu ikiwa na points 13 kama ilivyo miaka yote timu hizo kushika nafasi hiyo.

KMC akiwa nafasi ya nne na pointi 11, Tabora nafasi ya saba na pointi tisa, Mashujaa, Singida BS, Kagera na JKT zote zikiwa na pointi nane huku Ihefu ikiwa na pointi saba, Dodoma Jiji tisa na Geita Gold nafasi ya 13 na pointi tano.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: