Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mambo matano ya kuzingatia Simba kabla ya kuanza pre-season

Simba Zenzjis Mambo matano ya kuzingatia Simba kabla ya kuanza pre-season

Mon, 24 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Iko wazi kwamba Viongozi wa Simba wanapambana sana kurudisha heshima ya klabu hiyo na kuijenga timu upya lakini pia kurudisha Imani ya mashabiki na wanachama wa simba.

Lakini kabla ya Pre season kuanza Mnyama anatakiwa kuhakikisha mambo yafuatayo yanakamilika.

Kumaliza kuagana na wachezaji ambao wao viongozi wameona inafaa waondoke. Hili liwe kabla ya preseason kuanza ambapo hadi sasa zimetoka Thank You nne tu, ya John Bocco, Saidoo, Chilunda na Kennedy Juma.

Pili ni kumaliza usajili mpya kwa nafasi ambazo wao wanaona zinafaa kusajili. Hili liwe kabla ya Pre season kuanza Kwasababu itakuwa mbaya wachezaji wapya Kuja baada ya Pre season kuanza itaathiri ujenzi wa timu, yatajirudia ya msimu uliopita wachezaji wengine wanakuja kugundulika wana majeraha ya muda mrefu, timu inaingia gharama ya kuvunja mikataba na inakuwa imepoteza muda.

Tatu kuhakikisha benchi la ufundi liko vizuri na limekamilika kwa maana ya kupata makocha wenye uwezo mkubwa sana kabla ya kuanza maandalizi ya msimu mpya (Pre season).

Nne, kuhakikisha Kwa level ya uongozi Kuna utulivu Kwa kufanya vikao vyote vya umuhimu na kumaliza tofauti zilizopo kati ya upande wa 51% na 49% ili tutengenezee organization nzuri.

Tano, kuhakikisha pia ushiriki wa mashabiki (fans engagement) inarudi vizuri hii itawasaidi hata kujiandaa na tamasha kubwa la Simba Day haitakuwa ngumu kuwaita mashabiki.

Mambo haya matano Simba ikiyafanya vizuri kwa umakini basi huenda wasipate tabu kwa msimu ujao, kikubwa ni umakini kwenye usajili na kuwahi muda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live