Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mambo matano ya Benchikha Simba

Benchikha Simba Ms Mambo matano ya Benchikha Simba

Tue, 28 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Simba bado haina furaha baada ya juzi kuendeleza ilipoishia kwa kuanza kinyonge Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi ikilazimishwa sare ya bao 1-1, nyumbani na Asec Mimosas kutoka Ivory Coast huku ikionekana kucheza soka chini ya kiwango.

Matokeo hayo yalivuruga kuanzia kwa mashabiki, uongozi na wachezaji wenyewe lakini tumaini lao ni kocha mkuu mpya, Mualgeria Abdelhak Benchikha anayetarajia kuanza kazi rasmi kesho Jumatano au leo jioni.

Benchikha licha ya kuwa na wasifu, rekodi na ubora unaovutia lakini anakwenda Simba katika kipindi kigumu sana. Kipindi ambacho kila mtu ndani ya klabu hiyo kuanzia kwa mabosi, wachezaji hadi mashabiki wamechoka drama na hawaelewi nini kinawasibu lakini wanataka matokeo chanya tu.

Huenda, uzoefu na ubora wa Benchikha ukapunguza presha Msimbazi na kurejesha nuru katika nyuso za wakali hao wa Kariakoo lakini hata hivyo ili kuhakikisha hilo linatimia, kuna baadhi ya mambo anatakiwa ayafanye kwa umaridadi wa hali ya juu.

Mwanaspoti kupitia makala haya, linakuletea mambo muhimu saba, ambayo Benchikha anatakiwa kuyafanya katika msimu huu ili kurejesha furaha, ubabe na ufalme wa Simba katika soka la Afrika.

USHINDI

Simba imepoteza ari ya kushinda mechi siku hizi. Tangu imeifunga Ihefu bao 2-1 kwenye mechi ya ligi iliyopigwa Oktoba 28 mwaka huu haijashinda tena.

Imecheza mechi tatu mfululizo za kimashindano bila kushinda, ilianza kwa kuchapwa na Yanga 5-1, ikafuatia kutoa sare ya bao 1-1, na Namungo na juzi imetoa sare ya namna hiyo na Asec.

Ukiachana na hivyo, Simba haijashinda mchezo wowote wa kimataifa tangu msimu huu umeanza.

Ilianza kwa kutoa sare ya mabao 2-2 ugenini kwa Power Dynamos ya Zambia kwenye mechi ya kwanza ya mtoano Ligi ya Mabingwa Afrika, kisha ikatoa sare nyingine ya 1-1, nyumbani dhidi ya Wazambia hao na kufanikiwa kuingia makundi kwa sheria ya bao la ugenini.

Baada ya hapo ikashiriki African Football League na kutoa sare mbili dhidi ya Al Ahly ya Misri nyumbani na ugenini, ikianza 2-2 kwa Mkapa kisha 1-1, Cairo. Hapo kibao kiliigeukia na kuaga mashindano kwa kanuni ya bao la ugenini.

Iliyofuata ni mechi ya Asec ya juzi kwa Mkapa iliyoisha 1-1 huku Simba ikicheza hovyo.

Benchikha ana kazi kubwa ya kufanya hapo. Mashabiki na wadau wa soka nchini hawajaizoea Simba ikichechemea hivi, Simba ni timu ya ushindi na anapaswa kurejesha ushindi unyamani bila kujali atatumia mbinu gani. Akiweza hili atakuwa ameruka kiunzi cha kwanza pale Msimbazi.

KUFYEKA NA KUSAJILI

Pili ni hili la kufyeka na kusajili wachezaji wapya. Kwa bahati nzuri Benchikha anaingia Simba kipindi ambacho dirisha dogo la usajili linakaribia kufunguliwa.

Ukweli mchungu ni kwamba zaidi ya 75 asilimia ya wachezaji wa Simba wa sasa wamechoka, wengine hawastahili kuichezea timu namba nane kwa ukubwa Afrika.

Benchikha anahitaji kufanya tathimini ya kina na kuondoa wote ambao hawaendani na matakwa yake na klabu kwa ujumla bila kumuangalia mtu usoni wala kujali nani kaletwa na nani pale Msimbazi.

Hili litamuhitaji Benchika kuwa mtu chuma na mwenye misimamo haswa, kwani pale Simba kuna wachezani ni ‘Watoto Pendwa’ wa baadhi ya viongozi wa Simba.

Akimaliza hilo atakuwa na mtihani mwingine wa kusajili wachezaji watakaoendana na kasi ya soka la sasa, swali la atawapata wapi na fedha ya usajili ataitoa wapi, tumuachie yeye na uongozi wa Simba. Tusubiri kuona na kama atavuka kiunzi hiki vyema, Simba taratibu itaanza kurejea kwenye msitari.

KUUNDA TIMU

Jambo la tatu ni kuunda timu. Unajua kuna kuwa na wachezaji wengi, wazuri, wabovu, bora na wakawaida, harafu kuna kuwa na timu bora.

Benchikha anahitaji kuacha hayo yote bali atengeneze timu bora pale Simba. Hapa majibu yake atayapata katika kipengele namba mbili nilichokiandika ‘Kufyeka na kusajili’.

Timu ya Simba kwa sasa inachechemea, haina muunganiko, morali na ari ya upambanaji. Ni wachezaji wachache sana unaona wanapambana kwa ajili ya nembo ya Simba.

Hili ni jukumu la Benchika kurejesha yote yalitopotea ndani ya timu ya Simba na kuwa jeshi imara. Akifanikiwa hapa, huenda akaanza kupewa majina ya kizungu kama Proffesor, Master, na kadhalika.

KUREJESHA MASHABIKI UWANJANI

Jambo la nne ni hili. Nilikuwepo juzi uwanjani wakati Simba na Asec zinacheza, katika miaka ya hivi karibuni Simba haijawahi kucheza mechi ya kimataifa nyumbani huku jukwaani kukiwepo mashabiki wachache namna ile. Kwa Mkapa palipoa sana.

Haikuishia hapo, baada ya mchezo ule kumalizika, mashabiki wengi wa Simba walijuta kwenda uwanjani huku wengine wakiapa kutokwenda tena uwanjani kuitazama timu yao. Inafikirisha sana.

Hiyo yote inatokana na mwenendo mbaya, mashabiki hawaiamini timu yao tena, hawatambi tena, hawana furaha na wala hawaoni sababu ya kuwatoa nyumbani kwao, kulipa viingilio na kwenda uwanjani.

Benchikha anahitaji kufuta dhana hii kwa haraka sana. Na ni rahisi, anahitaji kufanya kwa usitadi mambo matatu tuliyoorodhesha juu kisha mashabiki watarejea uwanjani. Ushindi, usajili bora na timu imara ndivyo vitu vitawarudisha uwanjani maelfu ya mashabiki wa Simba walioikatia tamaa timu yao.

MATAJI

Jambo la mwisho ambalo linamsubiri Benchikha pale Simba na litamheshimisha zaidi ni mataji.

Simba katika misimu miwili mfululizo imepoteza mataji karibu yote iliyoyatwaa katika misimu minne nyuma. Si Ligi Kuu, Kombe la Mapinduzi wala Kombe la TFF (ASFC) yote yameyeyuka na mbaya zaidi kwao, mengi yamechukuliwa na mtani wake wa jadi, Yanga.

Ni Ngao ya Jamii pekee waliyoirejesha msimu huu chini ya kocha Robertinho aliyefutwa kazi, lakini mengine bado kivumbi na jasho.

Bwnchikha anasifika kwa makombe, huko Algeria na Tunisia wanamuogopa anapokuwa anawania taji, hivyo hivyo kwenye Kombe la Shirikisho Afrika na CAF Super Cup, huko kote amenyanyua makwapa kwa kubeba makombe. Sasa ni zamu ya kufanya hivyo akiwa Msimbazi.

Kama ataweza kutwaa walau Ligi Kuu msimu huu, itakuwa heshima kwake, akifanikiwa kubeba ASFC na Mapinduzi itamuongezea ‘Unyama’ na mwisho wa siku mashabiki wa Simba watamuona ‘Hana Baya’.

NGUVU YAKE KWA WACHEZAJI

Zipo taarifa kwamba ndani ya kikosi cha Simba kuna wachezaji ambao wana maamuzi kwa makocha wao kuanzia mazoezi makali wanayakataa lakini pia hata mamauzi mengine hili litamkabili Benchikha ni kwa namna gani atakuwa juu ya wachezaji wake ndani ya chumba cha kubadilishia nguo.

Benchikha ana nafasi kubwa ya kufanikiwa ndani ya Simba hasa ukizingatia yeye ni mtu mpya kama atakuwa na nguvu ya kulazimisha taaluma yake itangulie kuheshimiwa na kuibadili Simba basi atafanikiwa lakini akishindwa haya yanaweza kumkuta au kuamua kuachia ngazi, kazi ni kwake.

Chanzo: Mwanaspoti