Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mambo matano usiyoyajua kuhusu ubingwa ya Wananchi

Yanga Bingwa At 17 Mambo matano usiyoyajua kuhusu ubingwa ya Wananchi

Fri, 24 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wikiendi hii ni ya mabingwa, ndiyo ni wikiendi yao Wananchi katika kuelekea kusherehekea ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC walioubeba kwa mara ya tatu mfululizo, lakini pia mara 30 kwa ujumla.

Tayari ratiba ya kusherehekea ubingwa huo imewekwa wazi na sherehe zitafanyika kwa siku mbili mfululizo, Jumamosi na Jumapili.

Mwananchi hii siyo ya kuikosa kwani tayari utaratibu umeshawekwa kwamba kesho Jumamosi kwenye mchezo wetu dhidi ya Tabora United utakaochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa watakabidhiwa kombe letu.

Katika kuielekea Wikiendi ya Mabingwa, hapa kuna mambo kadhaa Mwananchi unayopaswa kuyafahamu.

1.CHOPPER ITAPITISHA KOMBE KATIKA ANGA LA DAR Halitakuwa jambo la kawaida kwani kombe wanalokwenda kukabidhiwa haliletwi uwanjani kienyeji, litapandishwa katika chopper na kuzungushwa mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam kabla ya kituo cha mwisho kuwa Benjamin Mkapa.

Huko mitaani litakapokuwa linapitishwa, wakazi wa Dar macho yao yote yatakuwa angani kulishuhudia kombe letu.

2.BURUDANI KABLA NA BAADA YA MECHI Wanachi mtajapokuja Benjamin Mkapa hamtakaa kinyonge kwani kutakuwa na burudani mwanzo hadi mwisho wa mchezo.

Burudani ambazo utazipata Mwananchi ni uwepo wa wasanii watakaoimba nyimbo mbalimbali huku Ma-DJ wakinogesha, haitaishia hapo, utaipata pia burudani uwanjani, si unajua kikosi chetu ndio kinaongoza kwa kutoa burudani uwanjani, sasa unakosaje kwa mfano.

Burudani hizi zitaanza mapema na mageti ya Uwanja wa Benjamin Mkapa yatakuwa wazi kuanzia saa 4 asubuhi, huku tayari viingilio vikitajwa kuwa ni Tsh 10,000 kwa Jukwaa la V.I.P B, V.I.P C Tsh 5,000 na Mzunguko Tsh 1,000.

3.SURPRISE KUBWA Hapa tuwekane sawa, viongozi wa Klabu ya Yanga wanaposema watafanya surprise basi utambue kwamba kuna kitu cha tofauti kitafanyika.

Hii haitakuwa surprise tu, bali imeandaliwa SURPRISE KUBWA.

4.PARADE KUANZA JUMAPILI Baada ya Jumamosi kukabidhiwa kombe letu na kusherehekea nalo pale uwanjani, shughuli itaendelea Jumapili kwa kufanya Parade la Ubingwa.

Parade hilo litaanzia Uwanja wa Benjamin Mkapa mapema tu asubuhi, watapita mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya Wananchi na wasiokuwa Wananchi kupata fursa ya kulishuhudia kombe letu, kisha kituo kitakuwa Makao Makuu ya Klabu Jangwani ambapo sherehe zitaendelea hapo.

Katika kuweka msisitizo, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Young Africans SC, Ally Kamwe, amesema: “Mnamo tarehe 26 Mei 2024 tutakuwa na Parade la Ubingwa, tutaanzia Uwanja wa Benjamini Mkapa kuanzia asubuhi kuja Jangwani. Najua miongoni mwa vituo vyetu mnavijua… Safari hii hatupiti tu, tutakaa hapo kwa muda.”

5.SUPU DAY Ubingwa huo Wananchi hawasherehekei kinyonge, Wananchi watapata fursa ya kupiga supu matata katika sherehe hizo za ubingwa.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Young Africans SC, Ally Kamwe, amesema: “Kabla ya Parade la Ubingwa siku ya Jumapili (25 Mei) tunatarajia kuwa na Supu Day ya kusherehekea Ubingwa hapo hapo Lupaso. Tumeshapata ahadi ya ng’ombe sio chini ya 8 hadi hivi sasa.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live