Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mambo manne yaliyoikwamisha Yanga Mapinduzi

Yanga Mambooooo Mambo manne yaliyoikwamisha Yanga Mapinduzi

Tue, 9 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Yanga imehitimisha safari yake kwenye mashindano ya Kombe la Mapinduzi ikiishia hatua ya Robo Fainali baada ya kupokea kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa APR ya Rwanda, juzi usiku kwenye wa Uwanja wa New Amaan Complex, hapa Unguja.

Kipigo hicho ni cha kwanza kwa Yanga kwenye michuano hiyo na ilishinda mechi mbili na sare moja kwenye hatua ya makundi na kukata tiketi mapema kwenda robo fainali.

Inawezekana Yanga ilipiga hesabu za kufika mbali, lakini kuna mambo manne yaliyowakwamisha na kufeli hesabu zao tofauti na wadau mbalimbali walivyoiona.

KIKOSI MSETO

Kwenye michuano hii Yanga haikuwa na kikosi cha kwanza na nyota wake 10 walikuwa kwenye timu zao za taifa kwa ajili ya fainali za Afcon na wengine wakiwa majeruhi.

Hii ilisababisha Yanga kutumia zaidi vijana na wengine wazoefu wa kikosi cha wakubwa ambao hawakuwa na nafasi ya kucheza mara kwa mara.

Inaweza kuwa moja ya sababu ya kufeli kwenye hatua hiyo kwani imefika ni ngumu na timu zinapambana kuwania Sh100 milioni za ubingwa.

UKUTA DHAIFU

Kukosekana kwa mabeki wao wanne huku Joyce Lomalisa akiwa bado hajakaa sawa, ni sababu nyingine ya kufeli kwa Yanga kwenye hatua hiyo.

Yanga iliathirika kwenye eneo hilo hasa mchezo wa juzi dhidi ya APR waliokuwa na ubora tofauti na michezo mitatu iliyopita.

Mabeki watatu Dickson Job, Bakari Mwamnyeto, Ibrahim Hamad ‘Bacca’ wako kwenye kikosi cha Taifa Stars pamoja na kipa wao Djigui Diarra aliye na Taifa lake la Mali huku Yao Akouasi akiwa kwao kwa ruhusa maalum.

Hii iliifanya Yanga kuwatumia Gift Fred na kinda Hamis Nanguka, huku upande wa kulia ikimtumia Kibwana Shomari na golini akiwa Aboutwalib Mshery anayerudi kutoka majeruhi.

Ukuta huu haukuwa na utulivu na mchezo wa juzi ubora wa APR hasa kipindi cha pili ulidhihirisha hilo na kama wangekuwa makini wangefunga mabao zaidi.

FALSAFA ZA GAMONDI

Chini ya Kocha Miguel Gamondi Kocha Nasreddine Nabi, Yanga ilionekana kuwa na muunganiko mzuri wa wachezaji na kuwa na daraja moja na alitenmgeneza namna tofauti kikosi chake na kila mchezaji alipata nafasi na kuonyesha ubora wake.

Kwa Gamondi ni tofauti na ametengeneza timu tishio lakini isiyo na mzunguko na baadhi ya wachezaji wameshindwa kuwa sawa na wale ambao wanaanza mara kwa mara.

Zawadi Mauya na Gift wameshindwa kuwa sawa na wale wanaoanza na hii imewafanya wafanye makosa mengi.

Mauya amefanya makosa baadhi ya mechi na chini ya Gamondi ikiwemo mechi ya juzi iliyoonekana kumshinda na kuzidiwa na vijana ambao walicheza kwa mara ya kwanza.

Kwa upande wa Gift, licha ya kuonyesha ubora kwenye michuano hiyo, ameshindwa kuwa na maamuzi ya haraka kuwahi kuzima mashambulizi tofauti na mabeki ambao wamekuwa wakianza mara kwa mara.

HESABU ZA SIMBA/AZAM

Kama ilishtuka vile. Yanga ni kama ilikwepa mtego wa kukutana na watani zao, Simba ambao wako fulu mziki huku wao wakitumia zaidi vijana.

Ni wazi hata mashabiki wameona ni wakati sahihi wa kutolewa kuliko kwenda kupata aibu ya kichapo kutoka kwa mtani hasa kwenye mchezo wa fainali.

Ingekuwa hivi; kama Simba ingeshinda jana dhidi ya Jamuhuri, ingekutana nusu fainali na mshindi kati ya Azam FC na Singida Fauntain Gate na kutokana na ubora wao na kikosi chao ni wazi kingefika fainali.

Kwa Yanga kama ingeshinda dhidi ya APR ingekutana na Mlandege nusu fainali na kama ingefika fainali ingekutana na Simba.

Ndipo hapo, kwa kikosi cha Yanga kinachoundwa na vijana wengi dhidi ya Simba iliyo sawa na inakosa mastaa wake watatu tu, ingeleta shida kwenye mchezo huo na wanaona ni wazi wangepigika na bora wameishia hatua hiyo.

Hata hivyo Yanga imewabeba zaidi vijana na iliamua kutumia ikiwa ni faida kwao kwa kuwapa nafasi ya kuonyesha ubora wao.

Kwa ubora huo ulioonyeshwa na baadhi yao kama Nanguka na Shekhan Ibrahim, ni wazi ina hazina ya vijana itakaowatumia kama ikitaka kwenye mechi kubwa.

Pia itatakiwa iwatunze kwani wameonyesha ni faida kwa klabu hasa wakipata timu kubwa zitakazowanunua kama kucheza Yanga itashindikana.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: