Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mambo manne yaliyobamba mechi ya Stars, Burundi

74383 Taifa+pic

Thu, 5 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

JANA Jumatano, timu ya Tanzania 'Taifa Stars' iliibana mbavu Burudi kwenye mchezo wa kusaka tiketi ya kupangwa kwenye makundi ya kushiriki kombe la Dunia mwaka 2022 huko Qatar baada ya kutoka sare ya bao 1-1.

Katika mchezo huo kuna mambo manne matata yaliyojili na kuzidi kugonga vichwa kwa mashabiki wa soka, Burundi na hata hapa nchini ambayo ni pamoja na makipa wa timu zote mbili wanakipiga kwenye kikosi cha KMC.

 

MAKIPA WOTE KMC

Juma Kaseja mlinda mlango namba moja wa Taifa Stars na KMC  lakini Jonathan Nahimana ambaye naye alikuwa kwenye kikosi cha jana ndio kipa namba mbili wa KMC,  kufanya makipa hao kuzidi kuonyeshana ubavu kila mmoja kwenye safu yake.

 

Pia Soma

Advertisement
MAKOCHA WOTE WARUNDI

Jambo lingine, makocha wote, Etienne Ndayiragije wa Taifa Stars pamoja na Olivier Niyungeko wote ni raia wa nchi moja (Burundi). Ndayiragije Amejizolea sifa kubwa tangu alipokuwa kwenye kikosi cha Mbao FC, KMC na sasa anakinoa kikosi cha Azam FC.

 

WAFUNGAJI WOTE UARABUNI

Kama ulikua hujui kuhusu mchezo wa jana, wafungaji katika mchezo wa huo, wote wanakipiga timu za Uarabuni, Difaa Hassani El Jadidi ndio timu anayoichezea, Simon Msuva ambaye alisawazisha bao katika mchezo huo huku Cedric Amissi naye akikipiga Al-Taawoun FC.

 

MANAHODHA WOTE UBELGIJI

Mbwana Samatta nahodha wa Tanzania anayekipiga KRC Genk na nahodha wa Burundi, Saido Berahino naye akikipiga S.V Zulte Waregem zote zinazoshiriki Ligi Kuu ya Ubelgiji na katika mchezo wa kwanza wa ligi, Berahino alitupia bao moja katika mchezo ambao walishinda 2-0.

Chanzo: mwananchi.co.tz