Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mambo manane Ligi Kuu Wanawake

Yanga Princesss Mambo manane Ligi Kuu Wanawake

Fri, 8 Dec 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kama ulikuwa ukiisubiri kwa hamu Ligi Kuu ya Wanawake (WPL) basi nikwambie msimu ndio unaanza na kila timu imejipanga kufanya vizuri.

Kama kawaida Mwanaspoti linakuletea vionjo mbalimbali lakini safari hii tunakuchambulia mambo manane wakati WPL ikianza ambayo msimu uliopita yalionekana na huenda yakajirudia.

NGAO YA JAMII

Ni kama kuna muendelezo wa mabadiliko kwenye ligi hiyo kwani msimu huu kabla ya kuanza ligi timu nne za juu zitashiriki michuano mipya ya Ngao ya Jamii kama ilivyo kwa wanaume.

Yanga Princess, Simba Queens, Fountain Gate Princess na JKT Queens ndio zitaanza hatua ya nusu fainali Desemba 09, mwaka huu na kumalizika Desemba 12.

Ukiachana na mashindano pia Ligi hiyo imekuwa ikikumbwa na changamoto za kupata wadhamini lakini sasa Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom itadhamini mashindano hayo na kwa namna hiyo inaweza kuwa fursa kwa wadhamini wengine kuwekeza kwenye ligi hiyo.

USAJILI

Si jambo la ajabu kwenye WPL timu kusajili wachezaji katika dirisha kubwa kisha wakakaa bila ya kucheza michuano yoyote hadi dirisha dogo likafunguliwa na timu kuanza usajili mwingine bila ya ligi kuanza.

Swali ni je? timu zinasajili wachezaji gani ilihali walionao hawajacheza Ligi au mashindano yoyote ukiachana na timu inayoshiriki Ligi ya Mabingwa na wengine wakiwa katika majukumu yao ya timu ya taifa?

Ni kipindi kirefu tangu msimu wa mwaka 2022/2023 utamatike Mei mwaka huu na hadi hapo hakuna chochote kilichoendelea zaidi ya wachezaji kukaa kambini.

Simba Queens hadi sasa imetambulisha wachezaji wanne wa kigeni huku Yanga Princess ikisajili wanane, wanne wa ndani na wengine kigeni na JKT nao wakiongeza watatu wote wa ndani.

WACHEZAJI MAJI KUPWAA

Achana na wachezaji ambao wanazitumikia timu zao za taifa kuna wale ambao wako kambini wakiendelea kufanya mazoezi bila kucheza mechi.

Kundi hilo litakuwa katika athari ya kushuka viwango kwani wanakaa ndani ya miezi nane bila kucheza mechi za kimashindano huku wengine asilimia kubwa huongezeka uzito.

“Hii inakuwa ngumu kwetu makocha, ratiba ibadilishwe kwa kweli ukiangalia kipindi chote hicho unakaa tu na wachezaji wengine wanazidi kilo na hata viwango vyao havieleweki,” anasema Masoud Juma, kocha Fountain Gate Princess.

JKT NA REKODI TAMU

Msimu uliopita umekuwa wa tofauti kwani JKT Queens ambayo ilibeba ubingwa wa WPL na kuchukua karibu tuzo zote za Kipa bora wa mwaka, Naijat Abas, Kocha Bora, Ally Ally, Mchezaji Bora Donisia Minja.

Ukiachana na rekodi hiyo pia ipo ya kufunga hat-trick 11, zilizofungwa na wachezaji saba huku tano zikifungwa na JKT kutoka kwa Donisia Minja(3) na Stumai Abdalla aliyefunga (2).

JKT imevunja rekodi ya Simba ya kufunga hat-trick tano kwani msimu wa mwaka juzi ilishinda mabao 5-0 dhidi ya Ruvuma Queens huku wachezaji wanne wakifunga mabao matatu kila mmoja.

Wengine waliofunga hat-rick ni Winfrida Charles (Alliance Girls), Joanitha Ainnembabazi aliyesajiliwa na Simba, Cynthia Musungu (Fountain), Blessing Nkor aliyetimka Yanga msimu huu na Jetrix Shikangwa aliyekuwa Simba kila mmoja akifunga moja.

SARE YA DERBY

Huenda msimu huu ukawa tofauti kwa watani wa jadi Simba na Yanga na ikashuhudiwa mechi za mabao kama ilivyowahi kutokea misimu miwili nyuma.

Msimu uliopita zilipokutana timu hizo kila mmoja aliambulia sare ya bao 1-1 nyumbani kwake tofauti na nyuma ambapo Yanga ilikuwa mnyonge kwa mtani wake.

Kwenye mechi 10 ilizokutana timu hizo Simba imeshinda mara nane, sare moja na kufungwa moja huku Yanga ikishinda moja, sare moja na kufungwa mara nane.

WAZAWA NA KIATU

Ndani ya misimu miwili mfululizo Simba Queens imeweka rekodi ya kubeba kiatu cha ufungaji bora na wote wachezaji wa kigeni.

Msimu wa 2021/2022, Asha Djafar ndiye alikuwa kinara wa kupachika mabao akitupia nyavuni mara 27 kwenye mechi 22 za Ligi lakini msimu uliofuata alishindwa kutetea nafasi hiyo na kuishia kufunga mabao manane kwenye mechi 18.

Na hilo limetokana na kusuasua kupata namba kwani alijikuta akicheza kutokea benchini na kutopata muda mwingi uwanjani.

Msimu wa 2022/2023, Simba ilibeba tena kiatu kupitia kwa straika wao Mkenya, Jentrix Shikangwa aliyefunga mabao 19, nyuma ya Donisia Minja wa JKT aliyetupia kambani mara 17.

Mara ya mwisho mzawa kubeba kiatu ilikuwa 2020/2021 aliyekuwa straika wa Yanga, Aisha Masaka ambaye kwa sasa anakipiga, BK Hacken ya nchini Sweden aliyefunga mabao 35.

Hivyo washambuliaji wazawa msimu huu watakuwa na kazi ya kurudisha kazi iliyofanywa na wenzao misimu miwili iliyopita.A

TIMUA TIMUA ZA MAKOCHA

Ni Fountain pekee kwa timu za ushindani ambazo mpaka sasa bado iko na kocha wake lakini wengine watatu wametimua na kuleta wapya.

JKT, Simba na Yanga wote wanaanza msimu kila mmoja akiwa na kocha mpya wengine wakitimua kwa kukosa matokeo mazuri.

Yanga ambayo kikosi chake kwa sasa kipo chini ya Mzambia, Charles Haalubono aliyechukua nafasi ya Sebastian Nkoma baada ya kuachana na wananchi hao kwa makuba-liano ya pande zote mbili.

Kwa upande wa Simba iliachana na Mganda, Charles Lukula baada ya kumaliza mkataba nao huku JKT ikiachana na Ally Ally ambaye alikosa leseni A ya ukocha mkuu ambayo ingemzuia kusimamia kikosi hicho kwenye michuano ya kimataifa.

VILIO VYA MAKOCHA

Kaimu Kocha Mkuu wa Simba, Mussa Mgosi anasema dirisha dogo kwa upande wa wanawake halina maana kwa kuwa bado hawajajua waliowasajili wana uwezo gani wa kuendelea nao au kuwaacha.

“Hii inaweza kuwa gharama kwa viongozi wa timu kama utasajili dirisha dogo, nafikiri bado ratiba haijawekwa vizuri sasa utakuwa unaongeza wachezaji halafu hujui viwango vyao?.” Anasema Mgosi.

Kocha upande wa Juma anasema; “Unaongeza wachezaji unafanya nao mazoezi miezi saba au minane, miezi inayofuata dirisha linafunguliwa sasa unajiuliza unasajili nini kwahiyo kuna haja ya ligi yetu kubadilika,” anasema Masoud

Chanzo: Mwanaspoti