Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mambo magumu Sokoine

IMG 20240211 WA0005 Mambo magumu Sokoine

Sun, 11 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Pamoja na uchache wa mashabiki waliojitokeza kuiwahi mechi ya Tanzania Prisons na Yanga,  lakini wamejikuta wakikwaa kisiki wakiishia nje ya geti baada ya milango kutofunguliwa.

Mchezo huo wa kufunga mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu unatarajia kupigwa saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Sokoine, jijini hapa ikiwa kila timu inasaka pointi tatu.

Timu hizo zinakutana zikiwa hazijapoteza mechi katika michezo minne nyuma, zimeshinda tatu na sare moja japokuwa Yanga anajivunia rekodi ya matokeo mazuri katika misimu minne dhidi ya mpinzani huyo.

Mara ya mwisho Prisons kupata ushindi kwa Yanga ni msimu wa 2018/19 ilipoilaza mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Sokoine na tangu hapo wamekutana michezo 12 wakipoteza tisa na sare tatu.

Mwanaspoti Online ambayo tayari ipo viunga vya Sokoine imeshuhudia milango yote ya uwanja wa Sokoine ikiwa imefungwa ikielezwa mashabiki wataruhusiwa muda mchache ujao.

Hata hivyo, licha ya idadi ndogo ya mashabiki waliokuwa mlango wa kuingilia wameonekana kuendelea kusubiri hadi muda wa kuruhusiwa kuingia.

"Kwa sasa bado haijaruhusiwa shabiki yoyote kuingia uwanjani, wasubiri hadi baadaye milango itakuwa wazi," amesema mmoja wa askari aliyepo mlango wa jukwaa kuu.

Chanzo: Mwanaspoti