Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mambo magumu! Nabi akalia kuti kavu Morocco

Nabi Far Rabbat Kocha Nabi

Tue, 4 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Inaelezwa kuwa mabosi wa Klabu ya AS FAR Rabat inayonplewa na Kocha wa zamani wa Yanga SC, Nassirdine Nabi wamemwambia Kocha huyo kuwa endapo timu itapoteza nafasi ya kutwaa Ubingwa wa ligi kuu ya Morocco (Botola Pro) basi atafungasha virago vyake.

Licha ya Nabi kuongoza Ligi hiyo tangu mwanzo wa msimu, lakini katika mechi za hivi karibuni hajapata matokeo mazuri na Klabu ya Raja Casablanca imeshakamatia usukani Botola Pro wakiwa na alama 69 huku FAR Rabat wakishika nafasi ya pili na alama 68 katika mechi 29 ambazo wote wamecheza.

Mchezo wa mwisho FAR Rabat alitoa sare ya bao 2-2 dhidi ya Moghreb Tetouan. Kwenye msimamo inaonesha katika michezo mitano ya mwisho, Rabat wameshinda mitatu, kipigo kimoja na sare moja wakati Raja wakishinda mechi zote.

Mchezo wa mwisho Raja Casablanca walishinda bao 1-0 dhidi ya mahasimu wao, Wydad Casablanca.

Msimamo wa Ligi uko hivi;

01 Mechi 29 mabao ⚽49 alama 69 __ Raja Casablanca

02 Mechi 29 mabao ⚽63 alama 68 __ FAR Rabat

03 Mechi 29 mabao ⚽37 alama 52 __ RS Berkane

04 Mechi 29 mabao ⚽33 alama 43 __ UTS

05 Mechi 29 mabao ⚽32 alama 43 __ FUS Rabat

06 Mechi 29 mabao ⚽30 alama 41 __ Wydad Casablanca

06 Mechi 29 mabao ⚽30 alama 41 __ OC Safi.

Mpaka sasa imesalia mechi moja kwa kila timu ili kuifunga msimu wa ligi hiyo, hivyo kwa takwimu hizo, michezo ya mwisho ndiyo itaamua nani Bingwa wa Ligi Kuu nchini Morocco.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live