Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mambo Magumu! Kocha mpya Azam Aomba Muda

Mohamed Badru Kocha mpya Azam Aomba Muda

Tue, 21 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KAIMU kocha msaidizi mpya wa Azam, Mohamed Badru ameweka wazi kuwa benchi lao la ufundi linahitaji muda zaidi ili kusuka kikosi kitakachokuwa na mwendelezo wa matokeo mazuri ya ushindi.

Azam Jumatatu iliyopita walitangaza rasmi kuachana na aliyekuwa kocha wao Mzambia, George Lwandamina ambaye aliuandikia barua Uongozi wa klabu hiyo akiomba kujiuzulu na nafasi hiyo kuchukuliwa na mkurugenzi wa ufundi, Abdihamid Moalin huku Mohamed Badru akikaimu nafasi ya kocha msaidizi.

Badru juzi Jumamosi alikuwa sehemu ya benchi la ufundi la Azam lililoiongoza klabu hiyo kwenye mchezo dhidi ya Mbeya City ulioisha kwa sare ya mabao 2-2.

Kocha msaidizi wa Azam, Mohammed Badru alisema: “Tunashukuru kwa matokeo ya sare ambayo tuliyapata kwenye mchezo wetu uliopita dhidi ya Mbeya City licha ya kwamba haukuwa mpango wetu.

“Licha ya kwamba hatukupata ushindi, lakini tunajivunia mabadiliko makubwa ambayo kikosi kimeyaonyesha mpaka sasa, tunaamini tukipata muda zaidi wa kuwa pamoja basi tutarejesha ari yetu ya ushindi.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live