Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mambo 7 Kuhusu Sadio Mane wa Senegal, Liverpool, Aligoma Kuitwa MFALME

Goal Sadio Mane 1s38p968zl1wi1mcjgyo5iqymu Sadio Mane

Tue, 8 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Sadio Mane ametimiza ndoto yake ya kihistoria ya kuisaidia timu yake ya taifa Senegal kushinda kwa mara ya kwanza taji la AFCON.

Mane ambaye ni staa wa Liverpool ana utofauti na mastaa wengi matajiri hasa katika matumizi ya fedha zake.

Ametokea familia ya kimasikini ambayo ilikabiliwa na changamoto nyingi.

Haya ni mambo saba kuhusu mshambuliaji huyo:

1. Alitoroka nyumbani ili kucheza soka Alikulia katika Kijiji cha Bambali nchini Senegal. Wakati huo familia yake haikumruhusu kucheza soka. Baba yake alifariki akiwa na umri wa miaka saba, alilelewa na wajomba zake.

Anatoka katika familia ya Maimamu wa Kiislamu.

''Baba yangu hakutaka nicheze mpira kwa sababu aliamini kwamba elimu ni muhimu kushinda mpira. Ilikuwa vigumu kucheza soka kwa sababu yeye hakutaka hivyo,” anasema Mane.

Mwaka 2008, akiwa na umri wa miaka 16, Mane aliitoroka familia yake na kuelekea Dakar ili kutafuta timu. Alipatikana na kurudishwa nyumbani, akaambiwa hatapelekwa shule mwaka uliofuta na kwamba atapatiwa fursa ya kuendelea kusakata soka.

2. Kazi ya jamii ya Kiislamu Inasemekana anatumia fedha nyingi kuwasaidia masikini katika maeneo mengi ya taifa la Senegal. Alitumia fedha zake kusaidia watoto wadogo mbali na kuwajengea nyumba na vyoo watu masikini. Mapema kanda ya video ilizua hisia huku wengi wakimsifu.

3. Alikuwa akimuigiza El Hadji Diouf Akiwa na umri wa miaka 10 wakati Senegal ilipotinga robo fainali ya Kombe la Dunia 2002 na fainali ya AFCON.

Wakati huo kikosi cha taifa cha Simba wa Teranga kilishirikisha Aliou Cisse, Khalilou Fadiga na El Hadji Diouf.

"Wakati huo Senegal ilikuwa na wachezaji bora zaidi,'' alisema Mane.

Rafiki yake wa utotoni, Luc, alisema Sadio alikuwa na mifano miwili ya kuigwa: "Wakati huo Sadio alikuwa anavutiwa na Ronaldinho, lakini pia alimpenda El Hadji Diouf, ambaye alitutia moyo sana kucheza soka."

4. Ujumbe wa Mane kwa Mohamed Salah na Naby Keita Katika siku za ufunguzi wa AFCON, Mane alirekodi ujumbe wa video kwa wachezaji wenzake wawili wa Liverpool, Mohamed Salah wa Misri na Naby Keita, mzaliwa wa Guinea.

Alisema: "Nina ujumbe maalum kwa marafiki zangu wawili, Nabi Keita na Mo Salah. Kwa bahati mbaya, katika fainali, hakuna timu mbili zinazoweza kukutana, hivyo ni lazima kucheza dhidi ya timu moja. Najua hilo. itakuwa Misri au Guinea, lakini najua nitawashinda mmoja baada ya mwingine."

Ajabu ni kwamba maneno ya Mane yalitimia na timu nyingine zote Afrika zilitolewa kabla hazijatinga fainali, na hatimaye moja kati ya timu mbili alizozitaja ni miongoni mwa timu zilizoingia fainali, Misri.

5. Baridi ilimnyoosha alipotua Ulaya Mwaka 2011, Mane aliondoka Senegal na kujiunga na klabu ya Ufaransa ya FC Metz. Kitu cha kwanza alichogundua alipokwenda Ulaya ni baridi.

Mane anazungumzia kilichompata yeye na wachezaji wenzake alipotoka kwenye vyumba vya kubadilishia nguo akiwa amevalia shati pekee. Alijua hali ya hewa ya Afrika mara nyingi ilikuwa ya joto."Wote walianza kunicheka na sikuelewa, lakini nilielewa baada ya kuingia uwanjani, baridi ilikuwa kali," anasema.

6. Ameshusha shinikizo la mashabiki wa Senegal Kwa muda mrefu, Mane amekuwa akionesha kiwango kizuri katika soka na klabu alizochezea zimenufaika na kazi yake, lakini amefanya machache kwa nchi yake.

Kwa hiyo, licha ya kupendwa na mashabiki wa nchi yake, walikuwa wakimshinikiza kuikuza Senegal.

Mnamo 2017, alishindwa kufunga penati ya kupeleka timu katika Robo Fainali ya AFCON. Mwaka 2019, hali ilizidi kuwa mbaya baada ya Senegal kupoteza fainali ya AFCON dhidi ya Algeria kwa bao 1-0.

Hivyo kwa taji la sasa ni wazi, Mane sasa amepunguza shinikizo kwa timu ya taifa, hiyo ni baada ya kuwa Mchezaji Bora wa AFCON na akafunga bao la mwisho la ushindi dhidi ya Misri katika fainali.

7. Akataa kuitwa mfalme Mara baada ya kubeba taji la AFCON, waliporejea Senegal kutoka Cameroon kuna mtu alimuita ‘MFALME’, lakini Mane akagoma kuwa yeye siyo MFALME.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live