Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mambo 10 yatakayosababisha Yanga akigwe na Simba Aprili 20

Simba X Yanga CAF Mambo 10 yatakayosababisha Yanga akigwe na Simba Aprili 20

Tue, 16 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga inatarajia kushuka dimbani Jumamosi, Aprili 20, 2024 katika Dimba la Mkapa kukipiga na watani zao Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC huku Wananchi wakiwa na kumbukumbu ya kumpiga mtani wao hamsa (5-1) kwenye mchezo wa mwisho.

Hii ni mechi ya wakubwa, mechi ya heshima, mechi ya historia kwa pande zote kuanzia mashabiki, wachezaji, mabenchi ya ufundi na hata uongozi wa kila timu. Kila mmoja anataka kutoka akiwa anatabasamu na kuzmodoa mwenzake.

Haya ni mambo yatakayoifanya Klabu ya Young Africans kupoteza mchezo ujao wa Dabi dhidi ya Simba SC.

Kila mchezo unaohusisha timu mbili ndani ya uwanja kuna anayeingia kama favorite (anayepewa nafasi kubwa ya kushinda) na kuna underdog (anayepewa nafasi ndogo ya kushinda).

Sasa ipo hivi, kutokana na muendelezo wa Young Africans kwenye michezo yote ya msimu huu yote ni story, ila kikubwa ni ile head to head ya Simba Vs Yanga (michezo iliyowakutanisha wenyewe kwa wenyewe).

Mchezo uliopita Yanga waliibuka na ushindi wa Magoli Matano kwa moja dhidi ya Simba, sio magoli tu, kiwango cha mchezo hasa kwa wachezaji wa Yanga kilikuwa juu sana, hakuna aliyekuwa na rating ya chini ya 7.4 hii ina maana kwamba wachezaji wote wamefanya kila kitu uwanjani kwa wastani wa zaidi ya asilimia 70 kila mmoja.

1. Yanga isipoheshimu mpinzani wake kutokana na hali anayopitia kwa sasa anapopata ugumu wa kupata matokeo, ukweli ni kwamba Simba hawachezi vibaya ila kwenye eneo la finishing ndo wameshindwa kuwa clinical.

2. Yanga ikibadilisha mfumo wake, siku zote faida ya timu kuwa na mfumo ni kuipa timu balance na Chemistry (uzani na muunganiko) hivyo basi mfumo ukibadilika muunganiko utapotea na tutaadhibiwa.

3. Non-stop Attacking: Namaanisha kuingia kwenye mchezo wachezaji wote wakiwa 'attacking minded', yani wote wanawaza kushambulia tu, wote wanapanda tu, hii itaacha mianya mingi na watafungwa kirahisi kwa counter attack.

4. Over confidence (kujiamini kupitiliza) Mechi waliyowafunga Simba goli tano walijiamini kupitiliza na wakawaadhibu vibaya, sasa wanasemaga "Karma is Real" Yanga wakifanya kama walivyofanya wao basi litawapata jambo.

5. Yanga isipojituma itawagharimu, dunia nzima hata kama timu ni bora vipi kama haitajituma basi kupoteza itakuwa rahisi sana.

Yanga wasahau yale matokeo yaliyopita wachezaji waipambanie nembo ya Club, mbali na hapo yatatokea kama ya Yanga na Azam, walijituma mwishowe wakapata matokeo kupitia Yanga.

All in all Kocha Gamondi wa Yanga ni mzoefu, haya yote anayajua, atajipanga kuja na falsafa na mipango mizuri ya kupambana na Benhikha kimbinu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live