Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mambo 10 usiyoyajua kuhusu usajili wa Musonda, TP Mazembe walizwa

Musonda Yanga Mambo 10 usiyoyajua kuhusu usajili wa Musonda

Sat, 14 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Yanga tayari wameanza mbwembwe. Baada ya jana kumtambulisha mchezaji mpya wa Kimataifa Kennedy Musonda kutoka katika klabu ya Power Dynamos ya nchini Zambia.

Leo kupitia katika ukurasa wa Afisa Habari wa Klabu ya Yanga Ally Kamwe ameandika;

Mambo 10 usioyajua, Usajili wa Musonda

1: Musonda ni Top Scorer wa Ligi ya Zambia. Mechi 17, Mabao 11. Ni mshambuliaji kinara wa Power Dynamos, ambayo inaongoza Ligi.

2: Power Dynamos ni klabu imara kiuchumi. Inadhaminiwa na kampuni moja kubwa ya kufua umeme pale Zambia. Ni msimu huu wamedhamiria kumaliza ukame wao wa mataji wa miaka 12. Kwanini wamefanya Deal kubwa hivi na Yanga?

3: Sifa ziende kwanza kwa Rais Eng Hersi Said ???? Kwanini? Kwanza, elewa kuwa TP Mazembe pia waliingia kwenye vita hii. Wanataka kuimarisha kikosi chao kwa ajili ya michuano ya Kimataifa, waliweka dau kubwa pia mezani.

4: Lakini Musonda ‘option’ yake ilikuwa Yanga. Kwanini? Wakati Mazembe wakiwasiliana kwa Email, Rais Hersi aliacha usingizi wake na kutafuta ndege usiku na kutua Kitwe, mazungumzo na Dynmos yakawa uso kwa uso. Bao la kwanza likaanzia hapo.

5: Nguvu ya ushawishi, nguvu ya Hela kwenye meza ya mazungumzo ikawa silaha kubwa kwa @caamil_88 mbele ya Dynamos na kukubali kumuuza mshambuliaji wao hatari.

6: Kuipiku Mazembe kwenye Usajili, ambao ni wapo kundi moja na Yanga kwenye kombe la shirikisho la CAF, Ni ishara ya Uongozi wa Yanga kumaster sanaa ya Soka la Afrika kuanzia nje ya uwanja.

7: Nini kimemfanya Musonda aikubali Yanga na sio Mazembe? Mradi wa Yanga ni mkubwa, na bila shaka kila mchezaji mkubwa angetamani kuwa sehemu ya mradi huu mkubwa.

8: Kumbuka, Musonda ameacha ndoto zake za kubeba kiatu cha ufungaji bora Zambia na kuja Yanga, sio jambo dogo kwa mchezaji kulifanya hili. Kuna kazi kubwa imefanywa na Rais wa Yanga????

9: Kitendo cha Yanga kuingia kwenye vita ya usajili ya vigogo wa Afrika ni ushindi pia kwa Ligi yetu ya Tanzania. Hersi ameiheshimiwa Ligi yetu na kuipa thamani kubwa. Hii deals itakuwa imefanya mawakala na wachezaji wengi wakubwa wajiulize kuna nguvu gani Tanzania.

10: Mashabiki wa Dynamos hawajaelewa ni nini kimetokea. Waandishi na mitandao ya Zambia imejadili kwa mshangao usajili huu. How is it Possible? Hawaamini kama Dynamos wameuza silaha yao kwa Yanga. Wakati wao wakishangaa, Wananchi wanafuraha ????

Chanzo: www.tanzaniaweb.live