Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mambo 10 Wydad vs Simba SC

Ayoub Simba Penatii Mambo 10 Wydad vs Simba SC

Sun, 10 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

1. Mchezo mkubwa wa kibabe wenye maafa kwa Simba, siyo ya Hanang tena ni ya mtaa wa Morocco yaliyoleta simanzi Msimbazi.

2. Palikuwepo na mtu mmoja kutoka nchi ya Uarabuni jina lake akiitwa Ayoub, ni mtu mnyoofu alijitenga na uovu ila shetani alimchongea kwa Moo ili afukuzwe Simba ila Ayoub aliokoa penalti Simba wakiwa ugenini. Aisee Ayoub top top performance kwa Ayoub, achana na penalti ya Jabrane, angalia ontarget ya Sambou Bouly Jr.

3. Viungo wa Simba, Ngoma na Kanoute wamecheza vizuri kimkakati kupush mashambulizi na kulinda kitimu nidhamu yao ilikuwa kubwa sana.

4. Simba ya Kocha Benchika imechangamka sana ni tofauti na ile ya Robertinho ambayo ilikuwa unamuona Kibu pekee ndo kachangamka hii hadi Onana ameanza kubadilika.

5. Waydady walimbana sana Kibu ambaye amekuwa silaha ya Simba kwenye mashambulizi na kupelekea timu kipindi cha pili ikose uhai na mashambulizi ya hatari kwa upande wa Simba kivipi?

6. Kibu akiwa hana mpira alifuatwa na mtu nyuma akipokea mpira alikabwa na watu wawili na hii ni kwa sababu Kibu ana nguvu na kasi muda wowote wangemuachia nafasi angewadhuru Wydad.

7. Yahya Jabrane na Lahtim wamewasumbua sana Simba, jamaa hawa wana uwezo mkubwa wa mchezaji mmoja mmoja kwa kasi na maarifa waliyonayo kwenye 1 vs 1 licha ya Jabrane kupoteza mkwaju wa penalti.

8. Inonga na Che Malone ni ulinzi uliofanya marking nzuri sana leo alipofanya makosa Inonga, Malone aliyasahihisha alipofanya makosa Malone, Inonga alikuwa nyuma yake waliweza kumdhibiti vizuri Bouly Jr hadi akatoka bila madhara.

9. Tangu msimu uanze sijaona Simba ikicheza mechi bora namna hii ya kibabe dakika zote japo matokeo kweli hawajapata ila Simba wamejituma sana kama timu wanastahili pongezi.

10. Zekaria Draoui dakika za jioooni anatoboa jahazi la Simba na kufanya jahazi lizame kwa maumivu makali mno wakiwa wamekaribia ng'ambo na kuchana mikeka ya watu aloo mpira hauna huruma.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live