Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mama Karume amfungulia kesi Mzee Magoma

Mama Fatma X Magoma Mama Karume amfungulia kesi Mzee Magoma

Fri, 9 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo, Agosti 9, 2024, imetupilia mbali maombi yaliyowasilishwa na Juma Magoma na wenzake, yaliyolenga kuundoa uongozi wa Klabu ya Yanga madarakani na kuweka kando tuzo na amri zote zilizotolewa katika hukumu iliyowapa ushindi.

Hakimu Mkazi Mfawidhi, Franco Kiswaga, alitoa uamuzi huo wakati wa kusikiliza marejeo ya shauri la maombi namba 187/2022, yaliyofunguliwa na Bodi ya Wadhamini ya Klabu ya Yanga. Katika uamuzi huo, Mahakama imekubaliana na madai ya Bodi hiyo kwamba wazee hao hawakuwa na sifa za kisheria za kufungua shauri hilo.

Zaidi ya hayo, Mahakama imeamuru Magoma, Geofrey Mwaipopo, na Abeid Mohamed Abeid kulipa gharama za uendeshaji wa shauri hilo kwa Bodi ya Wadhamini ya Klabu ya Yanga. Uamuzi huu unaweka mwisho kwa jaribio la kuondoa uongozi wa klabu hiyo, huku Bodi ya Wadhamini ikipata ushindi katika shauri hilo.

Mzee Magoma na wenzake walishinda kesi waliyokuwa wamefungua mahakamni hapo wakipinga uhalali wa Baraza la Wadhamini la Yanga.

“Sisi kwa maana ya kesi tumemaliza kesi rasmi, tutakuja mahakamani kudai gharama zetu lakini Mama fatuma Karume na Mzee Katundu wamsikitishwa sana na saini zao kutumika kwenye mwenendo wa kesi ambayo wao hawakuhusika. Hii ni jinai na wameshafungua kesi polisi na sisi kama klabu tutawasaidia kwenye masuala ya kisheria ili haki ichukue mkondo wake.

“Mama Karume mwenyewe na Mzee Katundu wameshachukuliwa maelezo yao na polisi, upande wa magoma na wenzake itabidi waitwe polisi wajielezee waliwezaje kutumia saini za watu bila kupata ridhaa ya kisheria ya wahusika wenyewe.

“Mama Karume ameshachukuliwa sampuli za sahihi na zile nyaraka zilizoonekana zimefojiwa zimeshapatikana kwa hiyo tumeachia jeshi la polisi lifanye kazi yake.

“Mashabiki waendelee kuisapoti timu yao, ile sintofahamu ya kina mzee magoma na wenzake imefutwa rasmi leo na hawana chao tena. Sisi kwa upande wetu tumemaliza hapa kinachofuata ni kufungua kesi kudai fidia ya gharama zetu ambazo tumezitumia," amesema Wakili Simon.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live