Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Malone, Inonga wampa jeuri Mbrazil

Inonga X Che Malone Mzuka Malone, Inonga wampa jeuri Mbrazil

Sun, 10 Sep 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Licha ya takwimu kuonyesha Power Dynamos ni tishio kipindi cha kwanza ikiwa nyumbani, kocha wa Simba, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ ametambia uimara wa ukuta wake akiamini vijana wake wanaweza kufanya kile ambacho kilitokea msimu uliopita Kitende huko Uganda.

Septemba 16, Simba itaikabili Dynamos katika mchezo wa pili wa hatua ya awali ya kufuzu makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika,

Takwimu Dynamos katika michezo tisa iliyocheza mwaka huu katika mashindano yote nyumbani, imeshinda minne na sare mara tano.

Wababe hao wamefunga mabao 14 huku tisa kati ya hayo yakiwa kipindi cha kwanza, wakiruhusu sita na manne yakiwa kipindi hicho ambacho wamekuwa hatari. Ni timu yenye uwezo wa kufunga na kufungika kipindi cha kwanza.

“Tumepata muda wa kuwafuatilia tumeona ubora na udhaifu wao. Naamini tunaweza kufanya kilichotokea Uganda dhidi ya Vipers, bila shaka watakuwa tofauti na ilivyokuwa kwenye tamasha la Simba Day tulipocheza mchezo wa kirafiki,” alisema.

Mara ya mwisho timu hizo zilipokutana katika mchezo wa kirafiki, Simba ilishinda mabao 2-0.

Katika mchezo ujao unaopigwa Ndola, Zambia, Robertinho atakuwa na faida ya kurejea beki wa kati Henock Inonga aliyekuwa akiuguza majeraha ya bega aliyoyapata kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Singida Big Stars.

George Lwandamina, mmoja wa makocha wakubwa Zambia ameuchambua mchezo huo akiamini timu ambayo itakuwa bora zaidi kimbinu inaweza kutinga hatua ya makundi. “Ni ngumu kusema timu gani inaweza kuvuka hatua hii.Huwa naamini kwenye maandalizi, ubora wa timu na mbinu vyote vinatakiwa kufanya kazi kwa pamoja, “ alisema kocha huyo wa zamani wa Yanga na Azam FC.

Simba inatakiwa kuwa macho na Andy Boyeli ambaye kwenye michezo tisa ya mwisho nyumbani, mshambuliaji huyo ametupia mabao saba.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: