Wakati Mali wakitua jana nchini Uganda tayari kwa mchezo wa mwisho wa kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia Qatar, wachezaji wa Mali wamegomea mazoezi.
Mali leo itashuka Uwanja wa ugenini wakipambana na Uganda katika mchezo wa mwisho wa Kundi E.
Taarifa kutoka nchini Uganda zinadai wachezaji wa Mali wamegoma kufanya mazoezi wakishinikiza uongozi wa Serikali yao na shirikisho lao kuwalipa posho wanazodai katika mechi zao tatu walizoshinda.
Hata hivyo Mali tayari imeshakata tiketi ya kuingia hatua ya mtoano ya mwisho wakiwa ndio vinara wa kundi lao wakifikisha jumla ya pointi 13, baada ya juzi kuwachapa Rwanda ugenini kwa mabao 3-0 wakifuatiwa na Uganda ambao wana jumla ya pointi 9 baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Kenya.
Mgomo huo unaweza kuwasumbua mabosi wa shirikisho la Soka Mali kutokana na endapo wachezaji hao watagomea mchezo wa kesho wanaweza kujikuta wanapokonywa matokeo ya ushindi katika mechi zao na nafasi ya kufuzu ikitua kwa Uganda wanaofuatia nafasi ya pili.
Mbali na mechi hiyo pia kutakuwa na mchezo wa Uganda dhidi ya Kenya wakiwakaribisha wanaoburuza mkia katika kundi lao Rwanda lakini matokeo hayo hayawezi kubadili chochote katika kuamua nafasi mbili za juu.