Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Malengo yetu ni kuvuka robo fainali CAFCl - Eng. Hersi

Hersi Yanga Gamondiz Malengo yetu ni kuvuka robo fainali CAFCl - Eng. Hersi

Wed, 24 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Klabu ya Yanga SC Eng. Hersi Said amefunguka leo Julai 23, 2024 kwa njia ya simu akitoa pongezi za dhati kwa wananchama wapya waliojiandikisha katika klabu ya yanga SC wanaoishi Nchini Afrika Kusini.

Eng. Hersi ameeleza kuwa klabu msimu huu imefanya usajili mzuri zaidi na bora hivyo mashabiki wasiwe na wasiwasi na kikosi, lakini pia ameeleza kuwa mojawapo ya amlengo ya klabu ya Yanga SC ni kuhakikisha wanaendelea kuteteta Ubingwa wa Ligi kuu Tanzania Bara pamoja na mashindano mengine ya ndani ya Nchi.

Eng. Hersi ameendelea kueleza kuwa kwa upande wa mashindano ya kimataifa kwa Mwaka jana klabu ya Yanga SC ilifanya vizuri zaidi ya kuyashinda yale malengo waliyoyapanga na pia malengo ya mwaka huu ni kuhakikisha wanafanya vyema zaidi ya mwaka jana 2023/24 katika mashindano hayo kwa kusonga mbele zaidi ya robo fainali.

Mwisho, Eng. Hersi amewaasa wanachama wa klabu ya Yanga SC kushiriki katika Shughuli mbalimbali zinazofanywa na klabu ya Yanga SC ndani ya Nchi na nje kwa ujumla lakini pia kuendelea kulipa ada mbalimbali za Uanachama ili kuchangia kurahisisha uendeshaji wa klabu hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: