Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Malengo ya Gamondi msimu ujao "Nataka nafasi ya tano"

Sac Gamondi Chama Dube Aziz Malengo ya Gamondi msimu ujao "Nataka nafasi ya tano"

Fri, 12 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga SC, Miguel Angel Gamondi amesema kuwa malengo yake ni kuifanya timu hiyo kuwa bora, tishio Barani Afrika na kuiweka kwenye nafasi tano bora za juu barani humo.

Gamondi amesema hayo baada ya kutua kambini Avic Town ambako kikosi chake kimeweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya ujao (pre-season) utakaoanza Julai 8, 2024.

“Mimi ni kocha ambaye ninataka mafanikio sio tu kushinda mataji bali kufanya vizuri ndani ya uwanja. Nafahamu tumefanya vizuri msimu uliopita lakini ninataka tufanye vizuri zaidi msimu huu, kwa hiyo ni lazima kuongeza uwezo wetu.

“Sababu iliyonifanya nikaja hapa msimu uliopita na ndiyo sababu iliyonibakisha msimu huu ni kwa kuwa ninataka kupambana kwenye mashindano makubwa Afrika na kuwaonesha kuwa Tanzania inaweza kufanya vizuri kwenye michuano mikubwa Afrika hususani CAFCL.

“Wakati tumemaliza msimu tulikubaliana tusisajili wachezaji wengi bali wachezaji bora ambao ni vijana na daraja la pili ambao ni wachezaji bora kwa ajili ya michuano ya Klabu Bingwa kwa sababu tunataka tufanye vizuri sana kwenye mashindano hayo, ninaiona Yanga kama moja ya timu bora na tishio Barani Afrika na malengo yangu ni kuwa miongoni mwa timu tano bora za juu Barani Afrika.

“Msimu uliopita tulicheza mechi na baadhi ya timu zilituogopa, lakini mechi zilikuwa ngumu sana watu hawajui tu lakini wachezaji wangu walikuwa anajituma sana na mpaka kuna mechi nyingine tulipata ushindi dakika za mwisho sana kwa sababu kila mchezaji alitaka tushinde kila mechi.

“Mimi ni kocha ninayetaka matokeo, sipendi kushindwa kabisa na kitu cha kwanza ninataka nidhamu kwenye kikosi changu hii sio kwa ajili yangu bali kwa ajili ya timu.

“Mimi ni Muargentina na Muitalia kwa kuzaliwa, asili yetu ni kupambana, ninataka wachezaji wangu wapambane hata kama wanafia uwanjani na timu yangu imeonesha hilo msimu uliopita. Tumecheza na CR Belouidad, Al Ahly na Mamelodi, wachezaji wangu walijituma sana kwenye hizo mechi, ninapenda kila mchezaji wangu ashambulie na kuzuia.

“Ninataka kila mchezaji apambane kupata nafasi, mimi siangalii jina kubwa la mchezaji bali kitu anachokifanya ndani ya uwanja. Unaweza kusajili jina kubwa lakini asicheze vizuri, lazima nifanye uchambuzi na kujua ni nani atacheza kwenye mchezo gani, kila mchezaji lazima nimjue.

“Kama kocha ninataka kupata kitu bora kwa kila mchezaji. Kwa sasa ninajenga timu yangu kwenye pre-season, kila mchezaji kwangu ni muhimu, wachezaji wapya wanatakiwa wanijue mimi ni kocha wa namna gani na ninataka nini.

“Mashabiki Wananchi wamekuwa wakitusapoti sana kila sehemu mpaka mikoani, wanalipa viingilio na kuja uwanjani kuisapoti timu yao, ni jambo kubwa sana na ninawapongeza, ninawaomba waendelee kufanya hivyo. Tunataka tuwe nafasi ya tano Afrika lakini hatuwezi kufika huko pasi na wao,” amesema Gamondi.

Aidha, Gamondi amesema mchezo walioalikwa nchini Afrika Kusini dhidi ya kaizer Chiefs (Kombe la Toyota), utamsaidia kukitazama kikosi chake, kujua uimara na mapungufu yake ili afanye marekebisho sahihi kabla ya msimu kuanza kwani anaamini itamsaidia kujenga timu bora kwa ajili ya mashindano ya ndani (Ligi Kuu, Kombe la Shirikisho, Ngao ya Jamii na Kombe la Mapinduzi) mashindano makubwa Barani Afrika (Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL na African Football League AFL).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: