Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Malale apania kuvunja uteja kwa Prisons

Malale Hamsini.png Malale apania kuvunja uteja kwa Prisons

Sun, 22 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha Mkuu wa JKT Tanzania, Malale Hamsini amepania kuvunja uteja unaoikabili timu hiyo kila inapokutana na Tanzania Prisons wakati zitakapokutana leo katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Katika michezo minane ambayo timu hizo zimekutana Prisons imekuwa ni mbabe zaidi kwani imeshinda minne, sare tatu na kupoteza mmoja.

Akizungumza na Mwanaspoti, Malale alisema licha ya kutambua ugumu wa mchezo huo, lakini wamejipanga kuhakikisha wanapata matokeo mazuri huku akiweka wazi kila mchezaji ana morali kubwa na anatambua umuhimu wa kuzipigania pointi tatu.

“Ni mchezo wa mtego kwa sababu siku zote unapokuwa ugenini ni lazima ujiandae kwa maana ya kiakili na kimwili na hii ni kutokana na kila timu inapigania kupata ushindi hivyo sio rahisi kwetu lakini tutaonyesha ubora tuliokuwa nao,” alisema.

Malale aliongeza kuwa licha ya kutokuwa na rekodi nzuri kwa Prisons, lakini hiyo haitakuwa sababu ya kuendeleza unyonge huo kwani wanahitaji kupata ushindi ambao utazidi kuwaweka katika mazingira mazuri wakati ligi ikizidi kusonga mbele kwa kasi.

Mara ya mwisho kwa JKT kuifunga Prisons ilikuwa ni ushindi wa bao 1-0, Oktoba 28, 2018, lililofungwa na nyota wa zamani wa timu hiyo, Anuary Kilemile.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: