Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Malalamiko kwa marefa ni unafiki

Kadi Pic Malalamiko kwa marefa ni unafiki

Fri, 22 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hatujawahi kuwa na msimamo na kilio cha pamoja pale marefa wanapokosea, zaidi tumekuwa tukijali masilahi yetu binafsi tu.

Simba ikinufaika na makosa ya refa, upande wa Yanga utamshambulia refa na upande wa Simba utamfurahia kwa kukumbushia matukio ambayo Yanga ilinufaika.

Yanga ikinufaika na makosa ya refa, upande wa Simba utamshambulia refa na upande wa Yanga utamfurahia kwa kukumbushia matukio ambayo Simba ilinufaika.

Azam ikinufaika, Simba na Yanga watamaind huku Azam ikikumbushia matukio ambayo Simba na Yanga zilinufaika. Azam ikiumizwa, Simba na Yanga watafurahia huku Azam ikinung’unika.

Kwa staili hii, wanaofanya makosa wanajiona wako salama na hawahisi kama wanatakiwa kuwajibika na hata wakikosea wanajua kuna upande utawasapoti.

Ipo mechi moja ambayo Arsenal waliwahi kunufaika na makosa ya refa, Mzee Arsene Wenger alisimama hadharani na kukiri Arsenal ilinufaika na makosa ya mwamuzi.

Wenger hakuweka video clips za mechi ambazo Man United, Chelsea na wengineo walinufaika. Alitanguliza masilahi ya soka mbele na sio ya timu yake. Anyway kupanga ni kuchagua.

Tuamue kuendelea na maisha yetu tuliyoyazoea au tuanze uwajibikaji wa pamoja. Vinginevyo tuendelee tu na unafiki wetu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live