Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makumbusho ya David Beckham kufunguliwa Marekani

David Beckham 163197068016x9 David Beckham

Sun, 19 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makumbusho mpya yenye lengo la kusheherekea maisha na mafanikio ya mkongwe wa soka David Beckham (47) inatarajia kufunguliwa nchini Marekani.

Baba mzazi wa nyota huyo,Ted Beckham (75) ambaye amekuwa akihifadhi vitu vingi sana tangu David akiwa mdogo ameahidi kuleta kumbukumbu hizo zote mahali hapo.

Makumbusho hayo yatakuwa katika ukumbi ilipo klabu ya Inter Miami inayomilikiwa na mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United.

Sehemu ya Makumbusho hayo inatarajia kuonekana katika mfululizo wa vipindi maalumu vitakavyoonyesha mambo tofauti yanayomhusu nahodha huyo wa zamani wa England na familia yake kwa ujumla.

Vipindi hivyo vitarushwa katika mtandao wa Netflix ndani ya mwaka huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live