Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makosa yaigharimu Stars

93d1556b3147383d27616175d5781ddc Makosa yaigharimu Stars

Thu, 21 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

KOCHA Msaidizi wa Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Selemani Matola amesema makosa madogo yaliyofanywa na kikosi hicho yamewaponza na kusababisha kuadhibiwa na Zambia katika mchezo wa kwanza wa fainali za Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (Chan).

Katika mchezo huo uliochezwa juzi nchini Cameroon inakofanyika michuano hiyo, Stars ilifungwa mabao 2-0.

Aidha, timu nyingine katika Kundi D, Guinea ilishinda mabao 3-0 dhidi ya Namibia na kuongoza kundi hilo, ikifuatiwa na Zambia, huku Tanzania na Namibia zikiwa hazina pointi yoyote.

"Ni makosa madogo sana kama ukiangalia, goli la kwanza ni penalti tulipofungwa tukaniki kutafuta goli la kusawazisha hivyo tukafanya makosa tukafungwa goli la pili,” alisema Matola baada ya mchezo huo.

Alisema mchezo kwa ujumla haukuwa mbaya kwani hata wao walipata nafasi kama ya Ditram Nchimbi ambaye kama angetulia wangesawazisha.

“Hayo yameshapita tunaangalia mechi ijayo namna ya kurekebisha makosa na kufanya vizuri,” alisema.

Kwa upande wake, nahodha wa kikosi hicho, Shomari Kapombe alisema haikuwa lengo lao kupoteza mchezo huo, lakini wameachana nayo na kujipanga kwa ajili ya mchezo unaokuja.

Alisema kilichowaadhibu ni kukosa umakini hasa kipindi cha pili ila ana amini mambo yatakwenda vizuri katika mchezo ujao.

"Tunamwachia mwalimu kurekebisha makosa yaliyotokea kujipanga na mchezo wa pili, ukiangalia tumecheza vizuri kipindi cha kwanza, kipindi cha pili umakini ukapungua tukaruhusu mabao mawili," alisema.

Stars ina kazi kubwa ya kuhakikisha inashinda michezo miwili iliyobaki ili kujihakikishia nafasi ya kuendelea katika hatua inayofuata.

Mchezo ujao itachuana na Guinea Jumatano ijayo

Chanzo: habarileo.co.tz