Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makosa ya udanganyifu, Cameroon hatiani kufungiwa AFCON ijayo

Alexandre Bardelli Makosa ya udanganyifu, Cameroon hatiani kufungiwa AFCON ijayo

Tue, 12 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwaka 2021 mchezaji wa Cameroon Nathan Douala alikuwa akiitwa Alexandre Bardelli alipokuwa mchezaji wa Oryx na wakati huo alikuwa na miaka 21.

Miaka mitatu baadae mchezaji huyo huyo badala ya kuwa na miaka 24 , umri wake ukarudi nyuma na kuwa na miaka 17 na ndipo akabadilisha na jina na kuanza kuitwa Nathan Douala akiwa mchezaji wa Victoria United.

Mchezaji huyu ambaye kuna utata kwenye umri wake na kujibadilisha jina alikuwa sehemu ya kikosi cha timu ya Taifa ya Cameroon kilichoshiriki AFCON 2023 akitumia jina la Nathan Doualla

Baadae mchezaji huyu na wengine 61 walifungiwa na Cameroon kosa lake likiwa ni kuongopa utambulisho

Kufuatia makosa hayo kuna dalili mbaya kwa timu hiyo ya Taifa kufungiwa kushiriki AFCON 2025 na 2027

Samuel Etoo pia atakuwa kwenye hatia kama Rais wa shirikisho na ameruhusu mchezaji mwenye majina mawili tofauti kuwa sehemu ya kikosi cha timu ya Taifa

Vifungu vya sheria vinavyoibana Cameroon

Article 45 reads “If CAF is informed, no matter the source, that a fraud or a forgery was committed by anymeans and /or support whatsoever by one or more national team(s), an investigation will be opened.”

Article 46 “In case the alleged facts are true, the national association concerned will be suspendedfrom participation in the following two editions of the AFCON”

Article 47 “For any administrative error in the registration of players, the national association concerned will be suspended from participation in the next edition of the AFCON, and itsteam will be eliminated from the competition if the latter is still on going.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live