Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Makosa binafsi yametugharimu"-Kim Poulsen

Kim Poulsen 1024x576 Kocha mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen

Fri, 12 Nov 2021 Chanzo: eatv

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mdernmark Kim Poulsen, amesema sababu kuu iliyoplekea kufungwa 3-0 dhidi ya DR Congo jioni ya Jana ni makosa binafsi ya safu ya ulinzi yaliyoadhibiwa kwa kufungwa mabao yote matatu.

“Kabla ya yote, Poleni sana kwa kupoteza mchezo leo. Kwasababu wote tulikuwa na matumaini makubwa kwenye mchezo wa leo. Nafikiri unaweza kuona kwenye mpira, utaadhibiwa kadri ukifanya makosa ukiwa unacheza kwenye michezo mikubwa".

"Tulifanyakosa baada ya dakika 6 na DR Congo wakaongoza na kuanza kujiamini. Tulienda mapumziko, tukajitahidi kucheza vizuri. Tulijaribu kujipanga upya ili kuwapa presha zaidi na zaidi lakini baada ya saa 1 tukafanya kosa lingine".

"Tukasababisha kona ambayo haikuwa na sababu ya kutokea kabisa. Lakini ninachotaka kusema ni kwamba, unaadhibiwa ukicheza michezo ya kuwania kufuzu kombe la Dunia na timu ambayo inashika nafasi ya 67 kwenye viwango vya ubora vya FIFA. Tunapaswa kupunguza makosa yetu, hiki ndicho tunapaswa kujifunza".

"Kila mchezo unapaswa kupata funzo, na tumejifunza kuwa ukitaka kushindana kwenye mashindano makubwa hutakiwi kuruhusu makosa ya namna hii tuliyofanya leo.

Kuwafunga DR Congo tulipaswa kuwa kwenye kiwango chetu cha juu kabisa cha ubora na hatukuwa hivyo leo kwasababu ya makosa binafsi".

"Tulipata nafasi lakini tulishindwa kuzitumia, kuzibadili kuzifanya mabao. DR Congo ni timu imara na yenye uzoefu. Nataka niwaambie kutoka moyoni, wachezaji walitaka sanaaa kucheza kwa kujitolea leo na sasa tumepoteza 3-0 kwasababu ya makosa binafsi".

Kwa matokeo hayo, Benin ndiye kinara wa kundi J akiwa na alama 10 akifuatiwa na DR Congo mwenye alama 8, Stars yatatu ikiwa na alama 7 zile zile ilhali Madagascar akishika mkia akiwa na alama 3.

DR Congo atashuka dimbani Novemba 14, 2021 kukipiga na Benin kwenye mchezo wa ‘Kufa au Kupona’ kwani sare itamfanya Benin kufikisha alama 11 na kusonga mbele wakati Ushindi kwa DR Congo utamfanya afikishe alama 11 na kusonga hatua ya mwisho ya mtoano.

Hatua inayofuata baada makundi kukamilika ni hatua ya mwisho ya mtoano ambayo itapangwa mwishoni mwa mwaka huu kupitia timu kumi zitakazofuzu na kucheza mtindo wa nyumbani na ugenini ili kutafuta wawakilishi 5 wa bara la Afrika kwenye michuano hiyo mikubwa Duniani.

Chanzo: eatv