Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makocha wazawa wachanwa ukweli

Image 377 1140x640 Minziro Felix.png Fred Felix Minziro

Tue, 31 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha mkongwe nchini, Almasi Shaban amelipongeza Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuwawezesha makocha kusoma kozi za soka la kisasa huku akiwataka wahitimu hao kutobagua mashindano na waache woga.

Shaban aliyewahi kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara akiwa na Majimaji ya Songea alisema makocha hao hawapaswi kuhitimu kozi hizo kubwa na kuishia kukaa mtaani bila kutumia ujuzi wao, hivyo wanatakiwa kusaka timu za kufundisha kusaidia soka la chini kuliko kuchagua tu kufundisha Ligi Kuu.

Kocha huyo ambaye kwa sasa anainoa Mwadui FC ya Geita inayoshiriki First League alisema baada ya kukaa pembeni kwa muda mrefu bila kufundisha ameamua kuchukua timu hiyo ya daraja la chini.

“Kozi za CAF zimeleta maendeleo ya kiufundi sasa makocha wengi wana uwezo mkubwa wa kufundisha mpira wa kisasa,nawaomba makocha hawa wanaohitimu hizi kozi na wana uwezo mkubwa wasione aibu na wasitake tu timu za Ligi Kuu, washuke huku chini tuzalishe vipaji vingi vitakavyosaidia kuvutia wadhamini kwenye hizi ligi za huku chini;

“Mwadui kuna vijana wazuri ambao wanahitaji mwendelezo na kukuzwa, kilichonisukuma kuja hapa ni kuona First League walimu wanakimbia nimeona nishuke huku nisaidie kuinua vipaji. Makocha wasione aibu warudi tufundishe huku chini tukuze mpira,” amesema

Kocha huyo mbali na kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara akiwa na Majimaji ya Songea amewahi pia kuzinoa timu za Tanzania Prisons, Polisi Dodoma, Polisi Mbeya, Polisi Morogoro na Milambo ya Tabora. Makocha wazawa wamekuwa wakilaumiwa kwa kushindwa kuthubutu kwenye miaka ya hivikaribuni na kuacha wageni wakitawala

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: