Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makocha watano wanaoweza kumrithi Klopp liverpool

Liva Pc Makocha watano wanaoweza kumrithi Klopp liverpool

Thu, 4 Apr 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya Jurgen Klopp kutangaza kwamba ataondoka mwisho wa msimu huu, Liverpool inahusishwa na makocha kibao. Majina mengi ya makocha yametajwa kwenye mchakato wa kuchukua mikoba ya Mjerumani huyo huko Anfield.

Baada ya makocha wengi kuhusishwa hii hapa ni orodha ya mabosi watano wanaoweza kwenda kurithi mikoba ya Klopp. Nani atachukua kazi?

5. Ruben Amorim

Ukiwaondoa Alonso na De Zerbi, huyu ndio anafuata kwa kupewa asilimia nyingi za kuchukua mikoba ya Klopp.

Taarifa kutoka The Mirror zinaeleza kwamba kocha huyo kutoka Sporting Lisbon pia anamezewa mate na Barcelona ili akachukue nafasi ya Xavi Hernandez.

Timu yoyote inayomhitaji itatakiwa kulipa kiasi kisichopungua Pauni 11.1 milioni ili kuuvunja mkataba wake unaomalizika 2026.

Kocha huyo kijana alifanikiwa kushinda taji la Ligi Kuu Ureno msimu wa 2020-21 akiwa na Sporting.

4. Julian Nagelsmann

Ukizungumzia makocha wanaofanya vizuri na vijana katika kipindi hiki huwezi kuacha kumtaja Julian Nagelsmann ambaye alianza kazi akiwa na umri wa miaka 28, alipokuwa kocha mkuu wa Hoffenheim kabla ya kutua RB Leipzig na baadae Bayern Munich.

Licha ya kushinda taji la Bundesliga, alifukuzwa mwaka mmoja uliopita na sasa anahudumu kama kocha mkuu wa Ujerumani akitarajiwa kuiongoza kwenye michuano ya Euro.

Kwa mujibu wa ripoti, mkataba wake na Ujerumani utaisha mara tu baada ya Euro kumalizika, hivyo kuanzia hapo anaweza akatua kwenye moja kati ya timu zinazomhitaji ikiwa ni pamoja Liverpool, ingawa Bayern Munich pia inahusishwa kutaka kumrudisha.

3. Ange Postecoglou

Moja kati ya mambo anayosifika nayo Jurgen Klopp ni uwezo wake mkubwa wa kuongoza wachezaji na uhamasishaji wake.

Hilo pia limeonekana sana kwa kocha wa sasa wa Tottenham Hotspur, Ange Postecoglou, aliyewahi kufanya hivyo akiwa na Celtic na anafanya sasa huko Spurs.

Tangu aichukue Spurs miezi minane iliyopita anaonekana kufanya sawa na kilichofanywa na Klopp alipoichukua Liverpool 2015.

Licha ya bajeti kuwa ndogo na kuondokewa na mchezaji tegemeo kama Harry Kane, kocha huyu ameiwezesha Tottenham Hotspur kuendelea kuwa timu shindani katika Ligi Kuu England.

Hata hivyo inaonekana kuwa ni ngumu kuondoka Spurs kwa sasa, lakini Liverpool ikiwekeza nguvu na kumpa ofa nono inaweza kumshawishi.

2. Simone Inzaghi

Makocha wachache ambao wana uhakika wa kunyanyua taji la Ligi Kuu Italia (Serie A) barani Ulaya msimu huu mmoja wao ni Simone Inzaghi, wa Inter Milan.

Katika siku za hivi karibuni Inzaghi ameshinda mataji matatu ya Coppa Italia na kuiwezesha Inter Milan kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kwa sasa ana mkataba na Inter Milan hadi Septemba 2025 na taarifa kutoka Italia zimefichua kwamba kuna mazungumzo ya kuurefusha zaidi yanaendelea.

Kutokana na uzoefu wake wa kufundisha timu kubwa kama Inter na kuipa mafanikio, Liverpool imevutiwa naye na tayari imeshaanza mazungumzo kwa mujibu wa The Mirror.

1. Pep Lijnders

Dakika kadhaa baada ya Jurgen Klopp kutangaza kwamba anaondoka Liverpool, zikaibuka raarifa nyingine kuwa msaidizi wake Lijnders naye ataondoka.

Lakini baada ya muda zikaibuka taarifa nyingine kwamba Lijnders ambaye aliwahi kufundisha NEC Nijmegen mwaka 2018 kabla ya kurejea Anfield anaweza akashawishiwa abaki kuongoza jahazi lililoachwa na bosi wake.

Hata hivyo, Ajax pia inaitaka huduma ya kocha huyu mwenye umri wa miaka 41.

Chanzo: Mwanaspoti