Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makocha wanaikimbia Man United

Rashford X Ten Hag Fresh Makocha wanaikimbia Man United

Tue, 9 Apr 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Ni kama kocha Erik Ten Hag sasa ameshusha pumzi baada ya presha ya muda mrefu juu ya hatma yake kwenye kikosi cha Manchester United.

Mholanzi huyu mwenye umri wa miaka 54, amekuwa akihusishwa kuondoka mwisho wa msimu huu ikiwa atashindwa kuiwezesha Man United kufuzu Ligi ya Mabingwa.

Hata hivyo, licha ya kutoonekana kuwa katika nafasi nzuri ya kufuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa mwakani kwa kumaliza ndani ya nafasi nne za juu, ripoti kutoka I News zimefichua Ten Hag hayupo katika hatari kwani makocha hawataki kuajiriwa na Mashetani Wekundu.

Kwa mujibu wa tovuti hiyo ni kwamba vigogo wa Man United tayari wameshaandaa orodha ya makocha ambao wanahitaji kuwaajiri lakini wote wanadaiwa kukataa.

Orodha hiyo inajumuisha makocha wakubwa kama Gareth Southgate anayeifundisha England na kocha wa zamani wa Bayern Munich ambaye kwa sasa anaifundisha Ujerumani, Julian Nagelsmann,

Chanzo kutoka I News kinaeleza Southgate alikataa kwa sababu ana wakati mzuri kwenye kikosi cha England ambacho kina vijana wengi wanaochipukia na aliangalia hali ya Mashetani Wekundu ambao kwa sasa inazidi kuwa mbaya.

Kwa upande wa Nagelsmann ambaye amesaini mkataba wa kuifundisha timu ya taifa ya Ujerumani amekataa kwa sababu yupo kwenye mazungumzo na chama cha soka nchini humo kwa ajili ya kusaini mkataba wa muda mrefu.

Zinedine Zidane anadaiwa kutohitaji kwenda kuishi England wakati kocha wa Brighton, Roberto De Zerbi naye havutiwi na kazi hiyo badala yake anaonekana kuwa nafasi kubwa ya kujiunga na Bayern Munich kwa ajili kuziba pengo la Thomas Tuchel ambaye anaweza kuondoka mwisho wa msimu.

Kocha wa Sporting Lisbon, Ruben Amorim ameonyesha kuvutiwa zaidi na Liverpool kwenda kuziba nafasi ya Jurgen Klopp mwisho wa msimu huu.

Makocha pekee waliobakia kwenye orodha ya matajiri wa Man United ni Graham Potter ambaye kwa sasa hana timu na kocha wa Brentford, Thomas Frank.

Chanzo: Mwanaspoti