Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makocha walioipa ubingwa Simba waibukia Botswana

Makocha Simba Makocha walioipa ubingwa Simba waibukia Botswana

Mon, 13 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha wa zamani wa makipa wa Simba na Yanga, Milton Nienov ameungana na kocha Didier Gomes da Rosa aliyewahi kuinoa Simba kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Botswana.

Milton ambaye alikuwa na Da Rosa Simba msimu wa 2020/21, alihamia Yanga mwaka 2021-23 na hakuwa na timu hadi alipojiunga na benchi la ufundi la Botswana chini ya Da Rosa ambaye aliongoza Simba kuingia hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2020/2021.

Milton ameposti picha yake akiwa na Da Rosa kwenye akaunti yake ya Instagram na kuandika “Nina furaha ya kufanya kazi tena na rafiki yangu mkubwa Didier Gomes, wakati huu katika timu ya taifa ya Bostwana kwenye kufuzu mashindano ya Kombe la Dunia 2026.”

Kipindi akiwa Simba, Milton alishiriki kuipa Simba mafanikio ikiwamo kushinda taji moja la Ligi Kuu la mwisho kabla ya ubabe kuhamia kwa watani zao Yanga, Ngao ya Jamii pamoja na Kombe la Shirikisho la Azam huku akiwa na Yanga aliisaidia kubeba makombe matano Ligi Kuu mawili Kombe la Shirikisho la Azam mara mbili na Ngao ya Jamii mara moja chini ya Kocha Nasreddine Nabi.

Botswana katika kufuzu Kombe la Dunia ipo kundi G na Algeria, Guinea, Msumbiji, Somalia na Uganda.

Chanzo: Mwanaspoti