Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makocha wa Ulaya wamimika Simba, 100 watuma CV kumrithi Pablo

Simba Sc Ceo Gonzalez Barbara R924u3yxx0511g9tf2b3fbsh4 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez

Tue, 7 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Simba imeachana na aliekuwa Kocha wake Mhispaniola Pablo Franco Martin wiki moja iliyopita baada ya kuondoshwa kwenye Kombe la ASFC hatua ya nusu fainali, lakini pia wakiwa na nafasi ndogo ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu.

Sasa tayari Simba wameshaanza mchakato wa kumsaka mrithi wa Pablo na Makocha kutoka sehemu mbali mbali wametuma CV zao wakiwania nafasi ya kukinoa kikosi hicho kwa msimu ujao.

Simba kwa sasa iko chini ya Kocha wake msaidizi Selemani Matola, na hii leo mtendaji Mkuu wa Simba Barbara Gonzales amedokeza mchakato huo ulipofikia;

"Tumepokea wasifu wa makocha zaidi ya 100 kutoka sehemu mbalimbali duniani ambao wengi wao ni kutoka barani Ulaya na Amerika Kusini. Mchakato wa mchujo unaendelea na tunategemea utakamilika ndani ya wiki mbili zijazo"

"Tunahitaji Kocha anayejua vizuri soka la Afrika pia tungefurahi kupata Kocha ambaye ni mzawa wa bara hili lakini mpaka sasa bado hawajatuma wasifu na aliteyuma mmoja na vigezo vyake havitoshi" amesema Barbara

Chanzo: www.tanzaniaweb.live