Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makocha 72 waomba kazi Yanga

Makocha Pic Data Makocha 72 waomba kazi Yanga

Thu, 11 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

By Thomas Ng'ituMore by this Author AFISA Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema tangu aondolewe  kocha Cedric Kaze na benchi lote la ufundi, wamepokea wasifu takribani 72  kutoka kwa makocha mbalimbali.

Kaze alifutwa kazi na benchi lote la ufundi baada ya kutoka sare 1-1 katika mchezo wao dhidi ya Polisi Tanzania.

Bumbuli amesema wameendelea kuzichakata CV hizo na bado makocha wameendelea kutuma.

“Si unaona ambavyo tulivyo bize yaani huko ndani watu wanaendelea kuchambua CV, tupo makini kuangalia kocha bora aje katika timu yetu”.

Bumbuli amesema katika makocha waliotuma CV hizo wapo ambao awali waliwahi kutuma na wengine wapya.

“Tunachoangalia ni uzoefu wa soka la Afrika na mafanikio, hilo ndio kubwa ambalo kamati ya Utendaji wanaangalia”.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz