Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makipa wa kigeni baadaye watakuwa tatizo kwetu

Diarra A0001 Makipa wa kigeni baadaye watakuwa tatizo kwetu

Mon, 18 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Moja ya timu za taifa zilizofanya vizuri sana kimataifa ni Misri na rekodi zao zimekuwa nzuri huku wakiendelea kuwatumia wachezaji wa nyumbani zaidi.

Misri wamekuwa na wachezaji wengi wa nyumbani ambao wamekuwa wakiiwakilisha timu yao ya taifa vizuri.

Bila ya ubishi ni kwamba hapa kuna uwekezaji mzuri zaidi au wa kipindi kirefu ambao umewafanya Misri kuwa na ligi bora.

Matunda ya ligi bora, yamewafanya kuwa na timu ya taifa nzuri ambayo inategemea nyumbani nan je kwa kiasi Fulani.

Kwa kipindi kirefu, uwekezaji wa Misri umekuwa na majibu mazuri na hili linapaswa kuwa funzo kwa timu nyingine za Afrika.

Wako ambao ambao zaidi wanategemea nje na hasa nchi za Afrika Magharibi, si kwamba hawajawekeza lakini wana mfumo tofauti kidog na Misri.

Mfano Senegal, kweli wamewekeza kwa kiasi kikubwa kwa vijana. Lakini wanachoangalia vizuri kwanza ni biashara na baada ya hapo faida kwa soka la Senegal na hasa tmu yao ya taifa.

Baada ya vijana kukua kisoka, wanahakikisha wanatoka katika mipaka ya Senegal na kwenda katika nchi nyingine zilizopiga hatua kisoka na hasa nchi za Ulaya. Wanajua baada ya muda kupitia idadi kubwa ya vijana, watakwenda kupata mafanikio kupitia vijana kadhaa ambao watakuwa na mafanikio makubwa.

Hapa nyumbani, mwendo wetu umekuwa si mzuri na tukubali kwa muda mrefu tumekuwa zaidi tukitegemea wachezaji kutoka Yanga na Simba kulingana na timu ina nini kwa wakati husika.

Hii itaenda inabadilika taratibu kulingana na muda, lakini wakati inabadilika tunaweza kuchukua mambo kadhaa, mfano kutoka Misri, kutoka Senegal au Magharibi mwa Afrika na kufanya mambo kadhaa ambayo yanaweza kutusaidia.

Moja ya kitu cha maana wanakifanya Misri au nchi karibu zote za Afrika Kaskazini ni kwa kuhakikisha wachezaji wa kigeni, hakuna nafasi kwa kipa wa kigeni au anayetokea nje ya nchi zao.

Wanajua faida zake, licha ya kwamba wana wachezaji wengi wa kigeni nje, lakini bado wanahakikisha nafasi ya kipa inaendelea kubaki kuwa ya wazawa.

Wanajua kipa anaweza kudaka mech izote au asilimia 90 za mechi za klabu kwa msimu mmoja. Hivyo kama atakuwa ni kipa wa kigeni kunakuwa ni kujinyima nafasi ya kutengeneza makipa bora wazawa.

Tanzania hatuna wachezaji wengi wa kigeni, hatuna kipa bora anayecheza nje ya Tanzania lakini bado sheria ya wachezaji wa kigeni, inaendelea kuwabana makipa hapa nyumbani.

Nimerudia mara kadhaa kuwa suala hili la makipa wa kigeni, tutakuja kuamka limeshatubana sana na kama tutakubali, huu ndio wakati wa kuamka na kuachana na kuwa na makipa wa kigeni.

Angalia, kama wachezaji wengi zaidi tunategemea kutoka Simba, Yanga au Azam FC, timu hizi kubwa za Tanzania, zote zina makipa wa kigeni.

Tena kwa upande wa Azam, kipa namba moja mgeni, namba mbili mgeni. Simba kipa namba moja kwa sasa ni mgeni kutoka Morocco kama ilivyo kwa Yanga kuwa na kipa wa kigeni kutoka Mali.

Maana yake, sisi tutaendelea kuyafaidisha mataifa mengine, mwisho yatawaita makipa wao kwa ajili ya timu za taifa kwa kuwa ndio wanaozitumikia timu zetu katika michuano ya kimataifa.

Wanafaidika wao, baadaye wanayafaidisha mataifa yao. Lakini wangekuwa ni wachezaji wazawa, mfano kwa hatua walizofikia Yanga na Simba kwa sasa, maana yake baada yah apo wangerejea na kuwa faida kwenye timu yetu ya taifa.

Tunapaswa kuanza sasa na si wakati mwingine, lazima tuangalia wakati ujao wa soka letu. Lazima TFF iliangalie hili na si lazima wanaosema wawe wale wenye kelele nyingi. Umuhimu wa hili utaonekana baadaye nav ema tuanze sasa kwa kuwa majibu ya hasara za hili, tumeshaanza kuyaona.

Makipa wengi wanaoitwa katika kikosi chetu cha timu ya taifa, wanakuwa ni makipa namba mbili kwa maana ya wale wasiopata nafasi au wale wanaocheza mechi chache. Tunapaswa kulifikiria hili mara mbili kabla ya wakati ambao tutaanza kulaumiana kuwa tulichelewa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live