Kazini kwa makipa wa Simba SC kuna kazi. Mstari huu aliwahi kuuandika mlinzi wa Yanga SC Kibwana Shomari akiuzungumzia uwezo wa mlinzi mwenzake Yao Kouassi.
Kazini kwa makipa wa Simba SC kuna kazi kweli. Pengo la kipa wao namba moja Aishi Manula limeonekana waziwazi, licha ya kukosekana kwa miezi saba sasa.
Lango la Simba SC haliko salama tangu Manula awe kitandani. Hivi sasa hakuna tofauti kati ya kipa anayeanza, anayekaa benchi hadi wengine wanaokaa majukwaani.
Kinachotokea sasa, Manula anayekaribia kurudi kiwanjani ameonekana kutamaniwa zaidi na mashabiki kuliko kawaida.
Makipa walioko sasa wametoa mianya kwa watu kumkumbuka Manula kwa baadhi ya matukio.
Kama makipa wale wangekuwa mahili Manula ingemchukua muda mrefu kurudi katika nafasi yake.
Kilichoko sasa. Nafasi yake bado inaonekana kuwa salama. Akiwa imara tu anarudi langoni kiurahisi tu.
Kama makipa wale wangekuwa imara ingemchukua muda mrefu Manula kupata nafasi yake. Lakini kinachoitokea Simba SC langoni mwake kumefanya wautamani urejeo wa Manula haraka.
Kuna makipa wamewahi kupata nafasi za kuwa makipa wa kwanza baada ya makipa tegemeo kuumia. Mifano iko mingi.
Lakini makipa wote wa Simba SC wameshindwa kuitumia nafasi hii. Sio Hussein Abel, Ally Salim wala Ayoub Lakred wote wametoa sababu za watu kumkumbuka Manula wao.