Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makata awafungia kazi Green Warriors Nyamagana

Pamba Jiji Mwanza Makata awafungia kazi Green Warriors Nyamagana

Thu, 12 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Wakati Pamba ikijiandaa kuwakabili Green Warriors keshokutwa Jumamosi, kocha wa timu hiyo Mbwana Makata amesema wanahitaji kukaza ili kupata ushindi mbele ya maafande hao ambao amedai huwa ni wagumu kufungika hivyo wanatakiwa kupambana sana.

Mchezo huo wa Ligi ya Championship utapigwa katika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza ambapo Pamba yenye pointi nane itakuwa na kibarua kizito cha kuwakabili Green Warriors ambao mpaka sasa wameshajinyakulia alama 10 kwenye mashindano hayo.

Makata alisema mchezo huo utakuwa mgumu kwao wapinzani wao anawajua ni wagumu kufungika hivyo ni lazima wapambane ndani ya dakika 90 ili kupata pointi tatu kwenye pambano hilo ambalo ni la nne kwao kucheza kwenye uwanja wa nyumbani.

Alisema hawataeleweka iwapo watashindwa kupata pointi tatu kwenye pambano hilo hivyo ameshawaambia wachezaji wake umuhimu wa mchezo huo.

"Timu Iko sawa kuwakabili Green Warriors nishawaambia wachezaji wangu umuhimu wa huu mchezo ambao kwetu utakuwa mgumu sana kutokana na aina ya klabu tunayocheza nayo hivyo ni lazima tukaze kama tunataka ushindi," alisema Makata na kuongeza;

"Mchezo uliopita tumepata pointi moja tu kitu si kizuri kwetu hivyo ni lazima huu mchezo tupate ushindi ambao utatufanya tuwe na alama 11 na kukimbizane na timu zilizo juu yetu kwenye msimamo wa ligi kitu ambacho kitafanya mechi kuwa ngumu."

Chanzo: Mwanaspoti