Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makata aanza kazi, atumia dakika 120

Makata Mbwana Akiwa Mbeya Makata aanza kazi

Mon, 21 Mar 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Baada ya kutua kikosini jana, leo Jumatatu Kocha Mbwana Makata ameanza kibarua chake kuinoa Mbeya Kwanza akitumia zaidi ya masaa mawili kujaribu ubora wa nyota wake.

Makata alitua jana jijini Mbeya na kutambulishwa kwa wachezaji ambapo leo ameanza rasmi majukumu yake akisimamia mazoezi yaliyofanyika kwenye uwanja wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia (Must) jijini hapa akiwa sambamba na aliyekuwa Msaidizi wake katika timu ya Dodoma Jiji, Renatus Shija na viongozi wa Mbeya Kwanza.

Hata hivyo haikuruhusiwa kufanya mahojiano yoyote huku Meneja na timu hiyo, David Naftar akiomba muda hadi kesho Jumanne watakapomtamburisha rasmi na kumkabidhi Jezi tayari kwa kuanza kazi.

"Kwa leo Kocha hataongea chochote kuna utaratibu tumeuweka kesho baada ya mazoezi Sokoine atatamburishwa rasmi na mtaweza kumuuliza chochote" amesema Naftar.

Pia hatma ya aliyekuwa Msaidizi kabla ya ujio wa benchi hilo jipya la ufundi, Nizar Khalfan itafahamika pia kesho wakati uongozi ukiendelea kuweka mipango sawa ya kuimarisha timu.

Kwa sasa Mbeya Kwanza inajiandaa na mchezo wake dhidi ya Biashara United utakaopigwa mjini Musoma mkoani Mara, April 6, ambao utakuwa wa kwanza kwa Makata kupambana kuinusuru timu hiyo iliyopo nafasi mbili za mkiani kukwepa kushuka daraja.

Wakati akihitimisha program yake, Kocha huyo wa zamani wa Polisi Tanzania, Alliance FC na Dodoma Jiji alisikika akiwataka wachezaji kujitambua na kuipambania timu ili kuipa thamani na kusahau matokeo ya nyuma na kuanza upya katika mechi zinazofuata.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz