Mchezaji wa Mashujaa FC, Said Makapu amezungumzia namna alivyopewa dhamana ya kushikilia kibarua cha kocha wa zamani wa Yanga, Luc Eymael baada kumwambia kuuwa mabosi wa timu hiyo hawakutaka yeye aanzishwe kwenye kikosi cha kwanza mchezo wa dabi 2020 dhidi ya Simba.
Beki huyo akifanya mahojiano na Mwananchi Digital amesema kocha huyo alipanga kikosi cha wachezaji 1o huku Kelvin Yondani alikuwa chaguo la mabosi ila kocha akaamua kuweka Imani kwake na kumuanzisha kwenye mchezo huo.
Ikumbukwe Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa kwa frīikiki na Bernard Morrison 'BM33 sekunde chache kabla ya mapumziko na kudumu mpaka mwisho wa mchezo.