Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makapu: Fei Toto nenda Ulaya sasa

Feisal  Toto khalid Aucho (kushoto) akiwa na Fei toto

Sun, 31 Oct 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Kitasa wa zamani wa Yanga ambaye sasa anakipiga ndani ya Polisi Tanzania, Said Juma Makapu, amesema anaamini kwa kiwango alichonacho kiungo wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’, ni muda wake sasa kwenda kucheza soka la kulipwa nje ya nchi.

Fei Toto amekuwa katika kiwango bora msimu huu. Mpaka sasa amefanikiwa kuhusika kwenye mabao matatu ya Yanga, akifunga mabao mawili na kuasisti bao moja katika michezo mitatu ya Ligi Kuu Bara pekee.

Makapu juzi Jumatano alikuwa sehemu ya kikosi cha Polisi Tanzania ambacho kilikubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Simba katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Makapu amesema: “Kwangu Feisal ni miongoni mwa viungo bora sana hapa nchini, na kwa kiwango ambacho amekuwa akikionyesha kwa sasa, bila shaka anastahili kupata nafasi ya kucheza soka la kimataifa nje ya nchi.

“Jambo la msingi kwake ni kuhakikisha anafanya sana mazoezi, kumsikiliza mwalimu wake na kuomba Mungu, naamini atatimiza malengo hayo.”

Chanzo: globalpublishers.co.tz